Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

Kristo sio tu mkuu kwa maana ya ukombozi wake bali kwa maana ya kuwa aina ya juu zaidi ya ufunuo. Kwa maana katika kulinganisha aina hizi mbili za ufunuo, Kristo ni mkuu na muhimu zaidi kuliko Maandiko kama ambavyo maisha ya mtu ni muhimu zaidi kuliko maelezo juu yake (k.m., katika wasifu). Hii haimaanishi kwamba Neno la Mungu lililoandikwa lisingeweza kuwa na thamani ya asili au ya ndani yake ikiwa halingemfunua Kristo. Neno la Mungu lingekuwa na thamani bila kujalisha linasema nini kwa sababu ya nani aliyelisema, yaani, Mungu ambaye ndiye chanzo kikuu cha thamani yote. Yesu alisema Maandiko “yalimhusu yeye mwenyewe” (Lk 24:27), au “niliyoandikiwa” (mst. 44), au “nimeandikiwa” (Ebr. 10:7), au “yanayonishuhudia” (Yh 5:39). Katika kila hali kusudi na thamani ya matokeo ya Neno lililoandikwa ni kwamba linamwasilisha Neno lililo hai la Mungu; matokeo ya umuhimu wa maelezo kuhusu Kristo ni kwamba yanadhihirisha nafsi ya Kristo. Kwa maana hii basi, Kristo ni mkuu kuliko Maandiko kwa sababu Yeye ni muhimu zaidi kuliko kauli zinazomhusu yeye mwenyewe. Pamoja na kuwa Maandiko ni ufunuo wa Kristo, mtu hapaswi kuyaheshimu maneno ya Biblia yenyewe, lakini badala yake, anapaswa kuyaheshimu kwa ajili ya Kristo—kwa sababu yanamzungumzia Yeye. Umuhimu wa Neno Lililoandikwa Ikiwa Neno lililoandikwa halina hadhi sawa na Neno lililo hai kama njia ya kumfunua Mungu, basi kwa nini Kristo alilipa mamlaka hayo (ona sura ya 1)? Kwa nini Yesu Mwenyewe mara nyingi alijenga msimamo wake na hoja zake juu ya msingi wa mamlaka ya Neno lililoandikwa (rej. Mt. 4:4 ff.; 5:17-18; Marko 7:6-8)? Kwa nini Maandiko yanarejelewa kuwa yamevuviwa na Roho wa Mungu (2 Tim. 3:16), kwamba hayawezi

133

Made with FlippingBook Digital Publishing Software