Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

kutanguka (Yh 10:35), wala kuondoshwa (Mt. 5:18)? Kwa nini kuna uwiano wa karibu sana kati ya sifa na kazi za Neno lililoandikwa na lililo hai? Neno Hai Ni Muhimu Kuliko Neno Lililoandikwa Biblia si “Papa wa karatasi.” Yenyewe kama ilivyo si ya kiungu; haipaswi kuabudiwa. Biblia si Mungu; inajumuisha maneno ya wanadamu ambayo kupitia hayo Mungu anazungumza. Ni Neno la Mungu, lakini limewasilishwa kwa kutumia maneno ya wanadamu. Kristo, kwa upande mwingine, ni Mungu (Yh. 1:1; Ebr. 1:8) na anapaswa kuabudiwa (Ebr. 1:6; Yoh. 5:23). Na kwa hivyo ulinganifu kati ya Biblia na Kristo si mkamilifu. Ni makosa kuona uvuvio wa Neno lililoandikwa na umwilisho wa Neno lililo hai kama dhana mbili zinazolingana kikamilifu. Si sahihi kuchukulia namna ambayo Mungu anajitangaza Mwenyewe katika maelezo ya Maandiko kuwa ni sawa na namna ambayo Mungu anakaa ndani ya utu wa Mwanawe. Maneno yenye ukomo, yenye mipaka ya Biblia yanatoa tu ufafanuzi wa kiini cha Mungu, wakati ambapo Kristo, ambaye ni Mungu, anatoa udhihirisho wake. Tunaweza kutolea mfano ufunuo wa Mungu katika uumbaji asilia. Mungu anajifunua kupitia uumbaji (Rum. 1:20; Zab. 19:1-) lakini Mungu hatakiwi kufananishwa na uumbaji kwa namna yoyote ile—hiyo ni ibada ya sanamu (Rum. 1:21-23). Vivyo hivyo, Mungu anajifunua kupitia Biblia, lakini haipasi kamwe kumlinganisha na Biblia—huo ni uabudu-Biblia. Yesu aliwakemea Wayahudi kwa kufananisha maneno ya Biblia na chanzo cha uzima wa milele. Walifikiri wangeweza kupata uzima wa kiroho ndani ya maneno ya Agano la Kale. Yesu alisema, “Mwayachunguza [kweli] maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake [si kupitia hayo kama njia tu ya kulifikia neno hali la Mungu]; na hayo [Maandiko] ndiyo yanayonishuhudia. Wala [kwa namna msivyo na ufahamu, mlivyo wapuuzi] hamtaki kuja kwangu mpate kuwa

134

Made with FlippingBook Digital Publishing Software