Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

na uzima [wa milele]” (Yh 5:39-40). 8 Walilijua ganda la Maandiko lakini walipuuza nafsi au kiini chake. Walichunguza, kama washirikina, ishara za Maandiko kana kwamba ni takatifu, na wakamkosa Mwokozi ambaye ishara hizi zilizungumza juu yake. Yesu alisema, “Kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu,” na “Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima” (Yh 5:46, 40). Uzima wa milele unapatikana katika Kristo na kupitia Biblia pekee. Umwilisho ni udhihirisho wa uzima huo (Yh 1:4), na uvuvio ndio njia ambayo kwayo tumepata rekodi yake yenye mamlaka (2 Pet. 1:20-21). NENO LILILOANDIKWA NI MUHIMU KWA NENO HAI Hili halihusiani kabisa na kusema kwamba mamlaka ya Biblia si muhimu au kwamba Maandiko hayana thamani muhimu bali yana thamani kama chombo tu (kadiri yanavyomwasilisha Kristo). Ni kusema tu kwamba wakati Biblia inapolinganishwa na Kristo kama njia mbili za ufunuo wa Mungu, uhalisi wa Kristo ni muhimu zaidi kuliko mamlaka ya Biblia. Uvuvio Ni Muhimu kwa Udhihirisho wa Mungu Kwa hakika, Maandiko ni yenye thamani si kwa sababu tu ni ufunuo kuhusu Mtu Mkuu (yaani, Kristo), bali pia kwa sababu ni ufunuo wa Mkuu Fulani na kutoka kwake (yaani, Mungu). Chochote ambacho Mungu anaeleza ni cha thamani, kwa sababu Yeye Mwenyewe ndiye chanzo na kiini cha thamani (rej. Yak. 1:17: 1 Yh 4:7-8). Na kwa kuwa Maandiko ni Neno au usemi wa Mungu, yana thamani hiyo, bila kujali yaliyomo au mada husika. Kwa hiyo, kile ambacho Biblia inasema ni muhimu kwa sababu ya nani alisema.

8 Tazama John Lange, Commentary on the Holy Scriptures: John . Grand Rapids: Zondervan), IX, 195.

135

Made with FlippingBook Digital Publishing Software