Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
Na sio tu kwamba Biblia ni muhimu kwa sababu ya nani aliyeisema, lakini haina makosa kwa sababu hiyo hiyo. Kwa maana Mungu hawezi kusema uwongo (Ebr. 6:18) au kufanya kosa (Zab. 18:30). Na kwa kuwa Maandiko ni maneno ya Mungu (2 Tim. 3:16; 2 Petro 1:20-21), basi ni dhahiri kwamba ni ya kweli na hayana makosa katika yote yanayofundisha. Kama Yesu alivyosema, “Maandiko hayawezi kutanguka” (Yh. 10:35), na “ Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka, hata yote yatimie” (Mt. 5:18). UVUVIO NI MUHIMU KWA UENEZAJI WA UJUMBE WA KRISTO Zaidi ya hayo, Maandiko yana thamani si kwa sababu tu ni ufunuo wa Mungu au hata kwa sababu ni usemi kumhusu Kristo, bali kwa sababu ni njia inayofaa ya kuhifadhi na kueneza Kweli hii. Bila shaka, Mungu angeweza kuchagua njia nyingine ya kuhifadhi na kueneza Kweli yake kuliko katika kitabu. Kimsingi, wakati wa zamani Mungu alisema “...na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi” (Ebr. 1:1). Nyakati fulani Mungu alizungumza kupitia (1) malaika (Mwa. 19); (2) ndoto (Mwa. 37); (3) maono (Dan. 7:1); (4) miujiza (Waamuzi 6:37); (5) sauti (1 Sam. 3:4-), (6) uumbaji-asilia (Zab. 19:1), n.k. Mungu angeendelea kujidhihirisha kwa njia hizi, lakini hakujiwekea kikomo namna hiyo. Badala yake, Alichagua kufanya ufunuo wake uandikwe katika maneno ya Maandiko, labda ni sababu hiyo hiyo ambayo inawafanya watu waandike maneno yao katika vitabu siku za leo, yaani kwamba ni njia sahihi zaidi ya kuyahifadhi na kuyaeneza. Njia nyingine mbadala ya uhifadhi andishi wa Kweli ni mapokeo ya mdomo au mwendelezo wake. Hata hivyo, mapokeo ya mdomo yana uwezekano wa kupotoshwa kwa urahisi, kama mtu yeyote ajuavyo ambaye amewahi kufuatilia hadithi kupitia mfumo wa mawasiliano kwa njia ya
136
Made with FlippingBook Digital Publishing Software