Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
“fununu na umbea.” Mapokeo ya mdomo kutoka kwenye midomo ya Kristo Mwenyewe wakati fulani yalipotoshwa ndani ya familia ya mitume wake waliomsikia akisema kwamba Yohana angeweza asife kabla Kristo hajarudi. Hili walilitafsiri vibaya kumaanisha kwamba Yohana hatakufa (Yh 21:23-24). Ikiwa kauli ya mdomo ilipotoshwa kutoka kwenye midomo ya Kristo hadi kwenye masikio ya mitume wake, ambao wangeweza kukosea katika mawazo yao binafsi lakini si katika mafundisho rasmi (Yh 14:26; 16:13), si zaidi kwamba kungekuwa na kiwango cha kutisha cha upotoshaji katika kipindi cha karne nyingi baadaye? Uhifadhi na uenezaji wa ukweli hufanyika kwa urahisi zaidi katika maandishi kuliko kwa njia ya mdomo. Wanadamu wanalijua hili, na ilifaa tu kwamba Mungu pia atumie njia hii kuhifadhi na kueneza Neno Lake. UVUVIO NI MUHIMU KWA UFASIRI WA UJUMBE WA KRISTO Hata hivyo, unyeti huu wa uvuvio wa Maandiko hauko tu katika suala la uenezaji bali pia katika suala la ufasiri wa ujumbe wa Kristo. Imejadiliwa kote katika kitabu hiki kwamba Kristo ndiye ufunguo wa ufasiri wa Maandiko (rej. sura ya 2). Ikiwa ni kweli kwamba Biblia inazungumza juu ya Kristo, basi kile inachosema kuhusu Kristo ni muhimu sana, na ni muhimu sana kuthibitisha ikiwa kile inachosema ni kweli au la. Ukweli huu ndio unaofanya mamlaka na uhalisi wa Biblia kuwa suala muhimu sana. Kwa maana ikiwa Biblia haitoi tafsiri yenye mamlaka na sahihi ya Kristo, kama inavyodai kutoa, basi inaweza kuwa na makosa na kupotoka pia; na mtu anawezaje kuwa na uhakika juu ya Kristo ikiwa ushahidi pekee alionao ni neno lisilo la uhakika kuhusu Kristo? (rej 1 Kor. 14:8). Kiwango cha mtu kumfahamu “Neno lililo hai,” ambaye anamtegemea kwa ajili ya uzima wa milele (rej. Yh. 8:24), kimewekewa mipaka katika njia ambayo kweli hiyo imewasilishwa kwake, yaani, Neno lililoandikwa. Inakubalika kwamba Biblia ni chombo tu ambacho Mungu hutumia
137
Made with FlippingBook Digital Publishing Software