Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

kuzungumza, hata hivyo, ujuzi wa mtu juu ya Kristo hupitishwa kupitia njia hiyo. Ikiwa mkondo si mkamilifu na una makosa, ndivyo ujuzi wa mtu juu ya Kristo utakavyokuwa usio mkamilifu na wenye makosa. Hata kama kweli andishi inatazamwa tu kama chombo cha kuwasilisha ufunuo binafsi [yaani Kristo], hata hivyo ujuzi wa mtu juu ya Mtu Mwenyewe (Kristo) ambaye anatambulishwa hautakuwa bora zaidi kuliko maelezo ambayo yanamtambulisha. Katika mfano mwingine, sahani ya santuri ikiwa mbovu au yenye michubuko, hata kama ina rekodi ya muziki uliopigwa na kurekodiwa kikamilifu na kwa ustadi wa hali ya juu, bado itatoa sauti mbaya. Kwa hiyo, utoshelevu wa ujuzi wa mtu juu ya nafsi ya Kristo umewekewa mipaka kwenye utoshelevu wa rekodi ambayo inamfafanua Mtu huyo kwake. Kwa maana utoshelevu wa ujuzi wa mtu juu ya Kristo si bora kuliko uhalisi na ukweli wa kumbukumbu ambayo inamwasilisha Kristo kwake. Bila shaka, mtu anaweza kusema kwamba Biblia haina makosa inapozungumza kuhusu mambo ya “kiroho” ambayo yanahusiana na Kristo, lakini akadai kwamba si kwamba haina makosa katika masuala ya kihistoria, uhakika wa taarifa au mambo yasiyo ya kimafundisho. Hata hivyo, kuna matatizo mawili ya msingi kwa mtazamo huu: (1) Mara nyingi haiwezekani kutenganisha masuala ya kihistoria na ya kiroho. Je, kuzaliwa na bikira kunaweza kumaanisha nini ikiwa Mariamu alizini? Ikiwa sio ukweli wa kibiolojia na wa kihistoria, basi kitheolojia ni hadithi ya kubuni pia. Je, kusulubishwa kunaweza kumaanisha nini kama hakukuwa na msalaba wenye damu? Ni upuuzi kusema juu ya ufufuo wa Kristo isipokuwa mwili wake kwa njia isiyo ya kawaida na ya kudumu uliondoka katika kaburi la Yusufu (rej. 1Kor. 15:17). (2) Zaidi ya hayo, imani ya mtu katika mafundisho ambayo hayahusiani moja kwa moja na ukweli wa kihistoria (k.m., mbingu, kutokufa), lazima ijengwe juu ya mambo fulani ambayo ni halisi na ya kweli kihistoria. Kwani mtu anawezaje kuyaamini Maandiko juu ya jambo ambalo halina uthibitisho wa kushikika au wa

138

Made with FlippingBook Digital Publishing Software