Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
kihistoria ikiwa Maandiko yenyewe yatathibishwa kuwa na makosa katika mambo ambayo kihistoria na kisayansi yamechunguzwa bila upendeleo? Kwa kuazima maneno ya Yesu, “Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, wala hamsadiki, mtasadiki wapi niwaambiapo mambo ya mbinguni?” (Yh 3:12). Mtu hafanyi makosa kusema na kuamini kwamba Neno lililoandikwa ni rekodi isiyo na makosa kuhusu Kristo, kwa maana Yesu mwenyewe alisema, “Maandiko hayawezi kutanguka” (Yh 10:35). Na tena akasema, “Amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka, hata yote yatimie” (Mt. 5:18). Sasa inatosha kusema kwamba ikiwa Yesu alithibitisha asili isiyo na dosari ya Agano la Kale ambayo ilimfunua kwa njia ya kutazamia tu, basi Agano Jipya, ambalo ni udhihirisho na tafsiri ya Kristo muhimu zaidi, pia ni kumbukumbu isiyo na makossa. Kristo ni ufunuo wa Mungu, kadhalika na Maandiko pia. Kama maneno ya Mungu, aina zote mbili za ufunuo wa Mungu zina thamani kubwa. Kwa kuwa, hata hivyo, kusudi kuu la Maandiko ni kuelekeza kwa Kristo, ufunuo wa Mungu katika Kristo ni muhimu zaidi kuliko ufunuo wa Mungu kupitia Maandiko. Lakini kama ambavyo taswira ya mtu kuhusu Kristo si bora kuliko picha iliyochorwa katika Maandiko, kila sehemu ya Kweli ya kimungu ni muhimu sana kwa mtazamo wa jumla wa mtu juu ya Kristo. Kutokana na hili, Mkristo anaweza kuridhika kujua kwamba popote anapogeukia katika Biblia atampata Bwana wake.
139
Made with FlippingBook Digital Publishing Software