Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

Ninampata Bwana wangu katika Biblia, Popote niangaliapo,

Yeye ndiye mada ya Biblia, Kiini na moyo wa Kitabu; Yeye ni Ua la Sharoni,

Yeye ndie urembo wa Yungiyungi, Popote ninapofungua Biblia yangu, Bwana wa Kitabu yuko hapo. Yeye, mwanzoni mwa Kitabu, Aliipa dunia umbo lake. Yeye ndiye Safina ya makimbilio, Inayobeba mapigo makubwa ya dhoruba Popote ninapotazama katika Biblia, Ninamwona Mwana wa Mungu. Kondoo dume juu ya Mlima Moria, Ngazi kutoka duniani hadi mbinguni, Kamba Nyekundu dirishani, Na yule Nyoka aliyeinuliwa juu, Mwamba uliopigwa nyikani, Mchungaji mwenye fimbo na gongo. Kichaka kinachowaka nyikani, Fimbo ya Haruni inayochipuka,

Uso wa Bwana ninaugundua, Popote ninapokifungua Kitabu.

Yeye ni Mzao wa Mwanamke, Mwokozi aliyezaliwa na Bikira Yeye ni Mwana wa Daudi, ambaye watu walimkataa kwa dharau, Nguo zake za fadhila na uzuri, yaani, staha ya Haruni. Lakini yeye ni kuhani milele, kwa maana ni Melkizedeki. Bwana wa utukufu wa milele Ambaye Yohana, Mtume, alimwona;

140

Made with FlippingBook Digital Publishing Software