Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
Mwanzo (Mwa. 1:27, taz. Mt. 19:4) hadi sura ya mwisho ya Malaki (Mal. 4:5, taz. Mk 9:12), Yesu kamwe hakunukuu au kurejelea vitabu vyovyote vya Apokrifa . Hakunukuu kamwe kitabu chochote isipokuwa vile ishirini na viwili vya Agano la Kale la Kiebrania, ambavyo vinalingana kabisa na vitabu thelathini na tisa vya Agano la Kale la Kiprotestanti. Nukuu za Yesu kutoka katika Torati Yesu katika jibu lake kwa Mafarisayo anarejea andiko la Mwanzo 1:27, “Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke…?” (Mt 19:4-5). Kutoka 16:4, 15 inanukuliwa katika Yohana 6:31: “…kama vile ilivyoandikwa, Aliwapa chakula cha mbinguni ili wale.” Yesu anarejea kitabu cha Mambo ya Walawi anapomwambia mwenye ukoma “ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa.” (Mt. 8:4, ling. na Law. 14:2). Yesu anarejelea andiko la kitabu cha Hesabu katika Yohana 3:14 anaposema, “Kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani...” (taz. Hes. 21:9). Katika vitabu vyote vya Torati, Kumbukumbu la Torati ndicho kitabu ambacho kilinukuliwa zaidi na Yesu. Alimpinga Shetani kwa nukuu tatu za Kumbukumbu la Torati (Mt. 4:4, taz. Kum. 8:3; Mt. 4:7, taz. Kum. 6:16; Mt. 4:10, taz. Kum. 6:13). Katika Marko 12:29, Yesu anataja kifungu maarufu cha Kumbukumbu la Torati 6:4 anaposema, “Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja.” Yesu pia alirejelea Kumbukumbu la Torati 24:1-4 kwa habari ya talaka, kadhalika na sheria ya jamaa wa karibu ya Kumbukumbu la Torati 25:5 (taz. Mt. 22:24), na nukuu nyinginezo. Pia, pamoja na ukweli kwamba vitabu vya Agano la Kale kama vile Esta na Wimbo Ulio Bora havijatajwa moja kwa moja na kuthibitishwa na Kristo, hata hivyo vilitimiza vigezo vya kikanoni. Nukuu za Yesu kutoka katika Vitabu vya Manabii Vitabu vya Manabii vilijumuisha sehemu iliyobaki ya Agano la Kale. Vitabu vingi vya kundi hili vilinukuliwa na Yesu. Yoshua na Waamuzi
23
Made with FlippingBook Digital Publishing Software