Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
au kurejea takriban vitabu kumi na tano kati ya vitabu ishirini na viwili vya kanoni ya Kiebrania ya Agano la Kale, vikiwemo vitabu kutoka kila sehemu, na mistari kutoka katika sura nyingi kuanzia sura ya kwanza ya Mwanzo hadi sura ya mwisho ya Malaki, lakini hakuna wakati wowote ambapo Yesu alinukuu au kurejea kitabu chochote cha Apokrifa. Kimsingi, kwa kuwa vitabu vya Apokrifa vilijulikana na Wayahudi wa siku za Yesu lakini havikuwa sehemu ya kanoni ambayo wao waliikubali (kama ambavyo Josephus anaonyesha wazi wazi), basi tunaweza, kihalali kabisa, kuhitimisha kwamba Yesu si tu aliviondoa vitabu vya Apokrifa kama sehemu ya kanoni ya Maandiko yaliyovuviwa lakini pia kwa hakika alijitenga navyo kabisa. Kwa ufupi, kanoni ya Kristo, kadhalika kanoni yenye vitabu ishirini na viwili (ishirini na vinne) iliyokubaliwa na Wayahudi wa Palestina wa siku zake, inafanana na vile vitabu thelathini na tisa vya Agano la Kale la Kiprotestanti la siku zetu. KRISTO: UFUNGUO WA UTHIBITISHO WA BIBLIA Si tu kwamba Kristo ndiye ufunguo wa uvuvio na uhalali wa kikanoni wa Biblia, bali pia Yeye ndiye ufunguo wa uthibitisho wa masimulizi ya kihistoria na ya kimiujiza ya Agano la Kale. Matukio mengi makuu ya Agano la Kale ambayo wakosoaji wa Biblia wanayapinga yalithibitishwa na Kristo. Hivyo, mtu atasalia na chaguo la ama kupinga uadilifu wa Kristo wa Injili au kukubali uhalisi wa matukio haya.
Uthibitisho wa Kristo kuhusu Uhalisi wa Kihistoria wa Matukio ya Agano la Kale
Yesu kibinafsi alithibitisha ukweli wa kihistoria kuhusu (1) Adamu na Hawa (Mt. 19:4); (2) Kuuawa kwa Habili (Mt. 23:35); (3) Nuhu na gharika (Lk 17:27); (4) Lutu na uharibifu wa Sodoma (Lk 17:29 ); (5) mababa wa Imani: Abrahamu, Isaka na Yakobo (Lk 13:28); (6) Musa na kijiti
25
Made with FlippingBook Digital Publishing Software