Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
Bado wakosoaji wengine wanadai kwamba Yesu hakujishughulisha na mambo yenye umuhimu wa kihistoria bali mambo ya kitheolojia au ya kiroho tu. Lakini sivyo ilivyo, kwani uthibitisho wake ulikuwa juu ya historia ya Agano la Kale na uhalisi wake, na mamlaka ya matamko ya Yesu ya kimaadili na kiroho mara nyingi yalijengwa juu ya ukweli kuhusu watu na matukio ya Agano la Kale ambayo aliyarejelea (Yh 8:56-58). Yesu alilijibu pingamizi hili aliposema, “Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani , wala hamsadiki, mtasadiki wapi niwaambiapo mambo ya mbinguni?” (Yh 3:12). Maana yake, ikiwa hatuwezi kuamini maneno ya Kristo juu ya mambo ya kihistoria yaliyonyooka, ambayo yanaweza kuthibitishwa kisayansi, tunawezaje kuamini kile anachosema juu ya mambo ya kiroho, ambayo hayawezi kuchunguzwa namna hiyo? Na Agano la Kale lenyewe ambalo Yesu alithibitisha uhalisi na mamlaka yake ya kimungu, limethibitishwa kupitia uvumbuzi mwingi wa kiakiolojia kuwa la kuaminika kihistoria. 5 KRISTO: UFUNGUO WA UFASIRI WA BIBLIA Hata miongoni mwa wale wanaokubali kwamba Kristo ndiye ufunguo wa vipengele vilivyotajwa hapo juu, inaonekana kuwa ukweli uliopuuzwa kwamba Yesu pia ndiye ufunguo wa ufasiri wa Biblia . Kristo, angalau mara tano, alisisitiza madai yake kwamba Yeye alikuwa ndiye kiini cha mawanda yote ya Maandiko ya Agano la Kale, na hata hivyo bado watu mara nyingi wanajifunza A.K. wakitilia maanani madokezo machache tu ya marejeo fulani ya kinabii na ya kitaipolojia (vivuli) kuhusu Mwokozi na kazi yake. Kurasa zinazofuata za kitabu hiki zitakuwa jaribio la kukuza na kuonyesha kwa usahihi jinsi Kristo anavyoweza kutazamwa kama ufunguo wa ufasiri unaofungua maana ya Biblia.
5 Ona Geisler na Holden, A Popular Handbook of Biblical Archaeology (Harvest House, 2013).
33
Made with FlippingBook Digital Publishing Software