Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
SURA YA 2 | KRISTO KATIKA AGANO LA KALE KULITAZAMA AGANO LA KALE KATIKA MSINGI WA KRISTO si suala la kiufasiri (kihemenetiki); kwa Mkristo ni sharti la kimungu. Katika matukio matano tofauti Yesu alijipambanua kama mada kuu ya Agano la Kale lote: (1) Mathayo 5:17; (2) Luka 24:27; (3) Luka 24:44; (4) Yohana 5:39; (5) Waebrania 10:7. Uchunguzi wa vifungu hivi unaonyesha kwamba kuna angalau njia nne tofauti za kulitazama Agano la Kale katika msingi wa Kristo. Kila kifungu kinasisitiza maana tofauti ambayo Kristo ni utimilifu wa Agano la Kale. Na katika kila kisa, kitabu ambamo tamko la Yesu linatokea ni kielelezo cha mtazamo huo wa kuliangazia Agano la Kale katika msingi wa Kristo. Vifungu hivyo vinasomeka kama ifuatavyo: • Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe (Lk 24:27). • Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi (Lk 24:44). • Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa) Niyafanye mapenzi yako, Mungu (Ebr. 10:7). 6 • Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza (Mt. 5:17). 6 Ingawa Waebrania 10:7 huenda ni rejea ya moja kwa moja ya kitabu cha Zaburi (40:8), ambapo nukuu imechukuliwa, na sio rejea ya Agano la Kale kwa ujumla, ukweli kwamba Masihi anasemekana kuwa alikuja kufanya lolote lile ambalo mapenzi ya Mungu yalielekeza, unahalalisha upanuzi wa rejea hii kwa Agano la Kale kwa ujumla wake, kadiri linavyofafanua mapenzi ya Mungu kwa ule utii wa kikuhani wa Kristo. Usahii wa mtazamo huu unaonyeshwa na utaratibu na mtiririko wa kitabu cha Waebrania chenyewe ambacho msingi wake ni kuufunua ukuu wa Kristo.
34
Made with FlippingBook Digital Publishing Software