Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

• Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia (Yh 5:39). Namna Nne za Kulitazama Agano la Kale katika Msingi wa Kristo

Mtazamo: Kristo Anatazamwa Kama Anayetimiza Agano la Kale

Kristo Anatazamwa kama Masihi na Mfalme Kuhani na Dhabihu Nabii na Mwalimu Mwokozi na Bwana

Ambapo Imeonyeshwa

Andiko

Luka na Matendo

Luka 24:27,44 Unabii wa Kimasihi

Waebrania 10:7

Ukuhani wa Kilawi

Waebrani

Mathayo 5:17 Sheria za Maadili

Mathayo

Yohana na Ufunuo

Yohana 5:39 Ahadi za Wokovu

KRISTO: UTIMILIFU WA UNABII WA KIMASIHI WA AGANO LA KALE Suala la kwamba manabii wa Agano la Kale walitabiri juu ya kuja kwa Kristo au Masihi linaweza kueleweka na kuthibitishwa kutokana na aya nyingi za Agano la Kale lenyewe, bila kutegemea utimilifu wa Agano Jipya. Waamini wa Agano la Kale walitazamia ujio wa Mwokozi tangu mwanzo kabisa (taz. Mwa. 3:15; 49:10), ingawa neno Masihi [aliyetiwa mafuta] lilitumiwa kwa mara ya kwanza kuhusu Mfalme wao ajaye katika 1 Samweli 2:10. Kwa hivyo, uchunguzi wa Agano la Kale ili kupata utabiri wake wa Kimasihi ni njia yenye msingi wa Kristo ambayo ni halali na yenye faida. Miongoni mwa maandiko yaliyovuviwa ya Agano Jipya inaonekana

35

Made with FlippingBook Digital Publishing Software