Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

kuwa ni Luka ambaye anatoa kielelezo bora zaidi cha jinsi utafiti kama huo unaweza kufanyika. Luka ndiye aliyeandika kwamba Yesu alithibitisha mara mbili uhalali wa njia hii (Lk 24:27, 44). Kwanza, kwa wale wanafunzi wawili waliokuwa njiani kuelekea Emau, Yesu alisema, “Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii! Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake? Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe ” (24:25-27). Wakiwa na ufunuo huu mpya, na maelezo haya ya kimungu ya Maandiko ya Kimasihi ya Agano la Kale yakiwa bado yanachemka mioyoni mwao, waliwapasha habari za matukio hayo wale kumi na mmoja (24:32-35). Kabla hawajamaliza kueleza, Yesu aliwatokea lile kundi, naye alipokwisha kula nao, akasema, “Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi” (Lk 24:44). Mara nyingi kumekuwa na maswali ya kutamani kujua ni nini hasa ambacho Yesu aliwaambia wanafunzi hawa na ni nini hasa kilikuwa maudhui ya mtazamo wake mwenyewe wa Agano la Kale katika msingi wa ujio wa Kristo. Lakini hakuna haja ya kujiuliza maswali mengi, kwa kuwa Luka anaonyesha wazi wazi mtazamo huo katika injili yake na katika kitabu cha Matendo. Mtazamo wa jumla, hata hivyo, ulitolewa kwanza na Kristo Mwenyewe kwa wanafunzi wale pale alipowafunulia “akili zao wapate kuelewa na maandiko. Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi….” (Lk 24:45-47). Hii inamaanisha kwamba Yesu aliwaelekeza kwenye unabii mkuu wa kimasihi wa Agano la Kale kuhusu kifo chake, ufufuo wake, na matokeo yake ambayo ni uinjilishaji wa ulimwengu.

36

Made with FlippingBook Digital Publishing Software