Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

Utabiri wa Kimasihi Ulionukuliwa katika Injili ya Luka Ni katika kitabu cha Matendo ambamo Luka anaonyesha vizuri zaidi mtazamo wa Kristo juu ya unabii wa Kimasihi, lakini hata katika injili yake kuna vifungu vingi. Luka anaelekeza kwenye ukweli kwamba Agano la Kale lilitabiri: 1. Huduma ya mtangulizi wa Masihi (Lk 1:17, taz. Mal. 4:5-6) 2. Jina la mahali alipozaliwa (Lk 2:11, taz. Mik 5:2) 3. Utambulisho wa Yohana Mbatizaji kuhusu Masihi (Lk 3:4-6, ling. na Isa. 40:3-5; Lk 7:27, ling. Mal. 3:1) 4. Tamko la Kristo katika sinagogi la Nazareti (Lk 4:18-19, taz. Isa. 61:2) 5. Kuingia kwa ushindi (Lk 19:38, rej. Zab. 118:26) 6. Kutakaswa kwa hekalu (Lk 19:46; Isa. 56:7; Yer. 7:11). 7. Jiwe Kuu la pembeni lililokataliwa (Lk 20:17, taz. Zab. 118:22) 8. Bwana wa Daudi (Lk 20:42, ling. na Zab. 110:1) 9. Mwana wa Adamu akirudi katika utukufu (Lk 21:27; Dan. 7:13) 10. Kristo akihesabiwa pamoja na wakosaji (Lk 22:37; Isa. 53:12) 11. Kuyapigia kura mavazi yake (Lk 23:34, taz. Zab. 22:18) Mingi ya mistari hii katika injili ya Luka inarejelea maisha na huduma ya Masihi. Katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Luka anarekodi matumizi ya utabiri mwingi zaidi wa Kimasihi, ambao mwingi unarejelea kifo na ufufuo wa Kristo na huduma ya injili kwa watu wa mataifa, bila shaka akionyesha kile ambacho Yesu mwenyewe alikuwa amewafundisha

37

Made with FlippingBook Digital Publishing Software