Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
wanafunzi kutoka katika Agano la Kale baada ya kufufuka kwake (Lk 24:46-47). Kwa maneno mengine, Luka anaonekana kueleza, kutokana na mahubiri ya mitume katika kitabu cha Matendo ya Mitume, mtazamo wa Kikristo ambayo Yesu mwenyewe aliwafundisha wanafunzi alipoonekana kwao baada ya ufufuo. Utabiri wa Kimasihi katika Kitabu cha Matendo Kitabu cha Matendo ya Mitume kinarekodi utabiri wa Kimasihi na utimilifu kuhusu: 1. Kumwagwa kwa Roho Mtakatifu (Mdo 2:17-21, kutoka Yoe 2:28-32) 2. Ufufuo wa mwili wa Kristo (Mdo 2:25-28 [rej. 13:35], kutoka Zab. 16:8-11) 3. Bwana wa Daudi (Mdo 2:34-35, kutoka Zab. 110:1) 4. Nabii kama Musa (Mdo. 3:22-23 [rej. 7:37], kutoka Kumb. 18:15, 19) 5. Baraka za uzao wa Ibrahimu (Mdo. 3:25, kutoka Mwa. 22:18) 6. Jiwe Kuu la pembeni lililokataliwa (Mdo. 4:11, kutoka Zab. 118:22) 7. Kukataliwa kwa Masihi kama Mfalme (Mdo 4:25-26 , kutoka Zab. 2:1-2) 8. Kondoo apelekwaye machinjoni (Mdo 8:32-33, kutoka Isa. 53:7-8). 9. Mwana aliyezaliwa kutoka kwa wafu (Mdo. 13:33, kutoka Zab. 2:7)
38
Made with FlippingBook Digital Publishing Software