Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

12. Baraka ya Ibrahimu (Gal. 3:8, kutoka Mwa. 12:3) 13. Laana ya msalaba (Gal. 3:13, kutoka Kum. 21:23) 14. Mzao wa Ibrahimu (Gal. 3:16, kutoka Mwa. 13:15; 17:8). Kwa hiyo, basi, Yesu alieleza kwamba Agano la Kale lilibeba utabiri wa Kimasihi kumhusu Yeye mwenyewe, na mitume, hasa katika kitabu cha Matendo, walionyesha kile ambacho Yesu alimaanisha kwa kusema hayo. Ufafanuzi zaidi wa mbinu hii unaonekana katika Warumi na Wagalatia, ambapo Paulo, ambaye Luka alishirikiana naye, anahusisha vifungu vingi zaidi vya Agano la Kale na Kristo. Orodha hizi hazimalizi unabii wa Kimasihi wa Agano la Kale; zimebeba tu baadhi ya vifungu vikuu vinavyohusu maisha, kifo na ufufuo wa Masihi na uenezi wa ujumbe wake. Kimsingi, zinaonyesha namna ambavyo Kristo alilifasiri Agano la Kale wakati alipowatokea wanafunzi wake baada ya ufufuo. Ikumbukwe hapa kwamba kauli ya Yesu kuwa Yeye ni utimilifu wa unabii wa Agano la Kale haikulazimishwa (kama Hugh Schonfield alivyosisitiza katika kitabu chake cha The Passover Plot ), kana kwamba alikuwa anajaribu, kwa makusudi au kwa udanganyifu, kufanya matukio ya maisha yake yaendane na utabiri uliotangulia awali kuhusu Masihi. Kwa hakika, unabii mwingi wa Kimasihi ambao ulitimizwa katika maisha ya Yesu wa Nazareti ulikuwa nje ya uwezo wake wa kibinadamu kabisa, kama vile: (1) mahali alipozaliwa (Mik 5:2); (2) wakati (Dan. 9:25-) na namna ya kuzaliwa Kwake (Isa. 7:14); (3) kukimbilia kwake Misri (Hos 11:1); (4) Utoto wake huko Nazareti (Isa. 11:1 , taz. Mt. 2:23); au hata (5) namna ya kifo chake (Zab. 22:16) na kitendo cha kuchomwa kwake mkuki ubavuni baada ya kufa (Zek. 12:10). Hata katika nyakati ambapo Yesu alikuwa na ufahamu wa kutimiza unabii wa Agano la Kale (k.m., Mt. 3:15; 5:17; 26:54),

40

Made with FlippingBook Digital Publishing Software