Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

hakuna ushahidi kwamba alibadilisha matukio ili kuonyesha sifa zake za Kimasihi. Badala yake, Yesu aliepuka kwa uangalifu kelele zozote kuhusu utimilifu wa unabii au utambulisho wake wa Kimasihi. Wakati wa ubatizo wake haikuwa Yeye bali ni sauti kutoka mbinguni iliyomtangaza kuwa Mwana wa Mungu (Mt. 3:17). Kugeuka kwake sura kulifanyika kwa ajili ya hadhira ya faragha ya wanafunzi wake watatu wa karibu zaidi (Mt. 17:1-). Wakati watu walipogundua wenyewe kwamba Yeye ndiye Masihi, Yesu “aliwakataza wasimweleze mtu… hata Mwana wa Adamu atakapokuwa amefufuka katika wafu” (Mk 9:9). Wakati fulani Yesu alikwepa majibu ya moja kwa moja kwa swali lililokuwa wazi la kama alikuwa Masihi au la (Yh 18:33- ; Mt. 11:4-5). Yesu alipotoa kauli za moja kwa moja kuhusu utume wake wa Kimasihi alizitoa katika mazingira ya faragha (rej. Yh. 4:26) au kwa wanafunzi wake tu (taz. Yh 16:28-29). Yesu alisema kuwa Yeye ni Masihi na Mwana wa Mungu, lakini hakuwahi kuonyesha uongo au ulaghai wowote wa kinabii wala hakujaribu kulazimisha matukio ya maisha yake kupatana na utimilifu wa unabii wa Kimasihi. KRISTO: UTIMILIFU WA UKUHANI WA AGANO LA KALE Yesu Kristo sio tu mada kuu na utimilifu wa Agano la Kale kwa maana ya Kimasihi pekee. Mtazamo mwingine wa Kikristo wa Agano la Kale ulibainishwa na namna Yesu alivyonukuliwa katika Waebrania 10:5-7 (kutoka Zab. 40:6-8). Katika kifungu hiki mkazo hauko juu ya kuja kwa Masihi au Mfalme mtiwa-mafuta bali juu ya Kuhani mkamilifu, si juu ya Yule anayetimiza matazamio ya Kiyahudi ya Mtawala bali Yule ambaye anawatengenezea nafasi kama Mpatanishi. Nukuu kamili inasomeka hivi: “Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema, Dhabihu na toleo hukutaka, Lakini mwili uliniwekea tayari; Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo; Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa) Niyafanye mapenzi yako, Mungu.” Ni

41

Made with FlippingBook Digital Publishing Software