Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

dhahiri kutokana na muktadha wa karibu hapa, na vilevile kwa kuzingatia muktadha wa kitabu kizima cha Waebrania, kwamba Kristo ameandikwa katika gombo la chuo cha Agano la Kale kwa maana ya kwamba anatimiliza ukuhani wa Walawi na mfumo wa dhabihu. Ni kweli kwamba kitabu cha Waebrania kinaongeza mistari mingi zaidi kwenye mkusanyiko wa unabii wa Kimasihi kama: • “Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele” (1:8, kutoka Zab. 45:6). • “Umependa haki” (1:9, kutoka Zab. 45:7). • “Mungu wako, amekutia mafuta” (1:9, kutoka Zab. 45:7). • “Wewe, Bwana, …uliiweka misingi ya nchi” (1:10-11, kutoka Zab. 102:25-26). • “Mwanadamu ni nini hata umkumbuke” (2:6-8 kutoka Zab. 8:4-6). • “Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu” (2:12, kutoka Zab. 22:22). • “Nitakuwa nimemtumaini yeye” (2:13, kutoka Isa. 8:17-18). Utimilifu wa Ukuhani wa Haruni Mkazo mkuu, hata hivyo, katika Waebrania ni juu ya utimilifu wa ukuhani wa Haruni kupitia Kristo, kama inavyoonyeshwa katika maelezo yanayofuata. Kristo Anakamilisha Mfumo wa Ukuhani wa Agano la Kale Ulinganisho wa ukuhani wa Haruni na ule wa Kristo utafunua kwa urahisi kwamba wote wawili wanafuata mfumo unaofanana. Kwa maana kile kilichofanyika kama kivuli katika mfumo wa ukuhani wa Haruni kilikamilishwa katika ukuhani wa Kristo.

42

Made with FlippingBook Digital Publishing Software