Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
Mfumo wa Walawi haukuwa mkamilifu na ulikuwa wa muda, na kwa sababu hiyo ulikuwa ni kivuli cha mfumo ambao ungekuwa kamili na wa milele. Mfumo wa kale ulikuwa ni kivuli tu cha kitu kinachopatikana katika kazi ya ukuhani ya Kristo; ulitoa kaida na taratibu, na Kristo alitoa uhalisi na ufanisi. Kristo Anatimiza Vivuli vya Hema ya Kukutania Sio tu kwamba ukuhani wa Agano la Kale ulikuwa kivuli cha Kristo, lakini hema na matoleo pia yalikuwa vivuli vya Kristo. Musa aliambiwa ajenge hema ya kukutania kwa kufuata kielelezo kilichofunuliwa kwake mlimani, kwa sababu hema ile ilitumika kama “nakala na kivuli cha patakatifu pa mbinguni” (Ebr. 8:5). Maana za vipengele vya hema hazijatolewa kwa undani (taz. 9:5) na mwandishi wa Waebrania, lakini Agano Jipya halimwachi mtu kuchanganyikiwa kuhusu ufafanuzi wa maana hizo kwetu. Yohana anatuambia kwamba “Neno [Kristo] alifanyika mwili, akakaa [kuweka maskani au ‘kupiga hema Yake’] kwetu” na “…tukauona utukufu wake” (Yh 1:14). Waebrania inatujulisha kwamba Yesu alifungua njia mpya na iliyo hai kwa mwamini “ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake” (10:20). Kwa msingi huu, imekuwa desturi miongoni mwa Wakristo kuhusianisha kati ya kazi za samani za hema la kukutania na Kristo. Elimu ya namna hiyo inaweza kwenda mbali hadi katika mambo ya kupita kiasi, lakini mtu angeonekana kuwa ndani ya mipaka salama ikiwa uhusianishaji huo utawekwa ndani ya mipaka ya kile ambacho Kristo mwenyewe anasema na ambacho Agano Jipya linasema kwa habari yake. Kristo Anatimiza Vivuli vya Hema ya Kukutania Vivuli vya Hema Tamko la Kristo Lango Moja Mimi ndimi mlango (Yh 10:9) Madhabahu ya Shaba Fidia kwa Wengi (Mk 10:45)
44
Made with FlippingBook Digital Publishing Software