Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
Ufafanuzi huu wa sikukuu katika msingi wa Kristo inaonekana unaenda zaidi ya kitabu cha Waebrania, lakini si zaidi ya mipaka ya Agano Jipya ya kile ambacho ni dhahiri kwamba kilimaanishwa katika Waebrania 10:5-7, kinaposema kwamba Kristo ndiye utimilifu wa mfumo wa ukuhani wa Walawi na taratibu za Agano la Kale .
KRISTO: UTIMILIFU WA SHERIA ZA MAADILI ZA AGANO LA KALE
Bado kuna namna nyingine ambayo Agano la Kale lote linamhusu Kristo, na hii inaonyeshwa katika Mathayo 5:17, ambapo Yesu anadai kuwa Yeye ni utimilifu wa sheria za maadili za Agano la Kale . “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii,” alisema Yesu, “Sikuja kutangua, bali kutimiliza .” Namna ambayo Kristo ni utimilifu wa Agano la Kale sio tu kwamba Agano la Kale lilitoa unabii wa moja kwa moja juu ya Kristo, kama ilivyokuwa mara nyingi katika unabii wa kimasihi. Wala Yeye si utimilifu wa Agano la Kale tu kwa maana ya kwamba alitimiza kile kilichokuwa kivuli katika mfumo wa sherehe. Maana ya tafsiri hii ya Kikristo ni pamoja na ukweli kwamba Yeye anakamilisha , anajaza , au anatimiza, sheria za maadili za Agano la Kale . Ni muhimu kutazama muktadha ambamo uthibitisho huu wa Yesu unafanywa. Ni katikati ya kanuni kuu za maadili za Hotuba ya Mlimani. Yesu ametoka tu kueleza Heri kuu za kimaadili (Mt. 5:1-11) na anakaribia utoa maana ya ndani, ya kiroho ambayo kwayo Agano la Kale linapaswa kueleweka (5:21-48). Lakini kabla tu Yesu hajatoa matamko haya makuu ya maadili kuhusu Agano la Kale, anawakumbusha watu kwamba hakuja kutangua bali kutimiliza Agano la Kale. Inaonekana wazi vya kutosha kwamba anamaanisha kwamba maisha na mafundisho yake yatatimiliza na kukamilisha mafundisho ya maadili ambayo Agano la Kale liliyatoa , lakini watu hawakuweza kuyafuata . Yesu hapa anatangaza kwamba kile
47
Made with FlippingBook Digital Publishing Software