Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
ambacho Agano la Kale liliagiza kimaadili atakikamilisha na kukitimiza kwa ukamilifu wote. Baadaye, Mtume Paulo aliona ukweli huu na kuandika, “Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili; ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.” (Warumi 8:3-4). Yaani, maagizo ya sheria za maadili, ambazo zilikuwa ni kiakisi cha tabia ya Mungu isiyobadilika na ambazo zilikuwa zimejumuishwa na kuagizwa katika sheria ya maadili ya Musa, zilitimizwa kikamilifu na Kristo, na kwa sababu hiyo kwa neema zinaweza kutekelezwa kwa mwamini. Yesu alitangaza wakati wa ubatizo wake kwamba ilikuwa nia yake “ kutimiza haki yote” (Mt. 3:15), na kisha katika mahubiri yake makuu anatangaza nia yake ya “ kutimiliza ” Torati na Manabii. Matamko yote mawili yana maana moja ambayo kwayo Kristo ni jumla ya Maandiko ya Agano la Kale, yaani, Yeye ni utimilifu au ukamilifu wa kanuni zake za maadili . Funguo Mbili za Namna Mathayo Alivyolifasiri A.K. katika Misingi wa Kristo Maneno mawili muhimu katika tafsiri ya Mathayo ya A.K. katika msingi wa Kristo ni haki (au mwenyehaki ) na kutimiliza . Maneno haya “Haki” au “ mwenyehaki ,” kwa mfano, yametumika takribani mara ishirini na tano katika injili ya Mathayo. Kinyume chake, maneno hayo yametumika mara kumi na tisa tu katika Injili nyingine tatu kwa pamoja. Mathayo anamzungumzia Yusufu kuwa mwenye haki (au mwadilifu, 1:19). Anaeleza kuhusu jua na mvua kwa wenye haki (5:45); kwamba Kristo hakuja kuwaita wenye haki (wenye kujihesabia haki) kutubu (9:13).
48
Made with FlippingBook Digital Publishing Software