Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
Anazungumza juu ya kumpokea mwenye haki na ujira wa mwenye haki (mara tatu, 10:41); juu ya wenye haki (13:17, 43, 48); matendo ya haki (20:4, 7); haki ya nje, yaani ya hadhara (23:28); juu ya makaburi ya wenye haki (23:29). Anaandika kuhusu damu ya mwenye haki (mara mbili, 23:35); wenye haki wakati wa kurudi kwa Kristo (25:37, 46); Kristo mwenyewe (27:19, 24). Haki inarejelewa kuwa (1) kile ambacho Kristo alikuja kutimiza (3:15); (2) kile ambacho wengine walikitamani (5:6); (3) kile ambacho kwacho wengine waliteswa (5:10); (4) kile ambacho katika kukitimiza ni lazima kuwazidi Mafarisayo (5:20); (5) ambacho yampasa mtu akitafute (6:33); (6) njia ya maisha (21:32). Kutokana na vifungu hivi ni rahisi kuona kwamba Yesu alikuwa akiwaita watu kutoka katika njia yao ya kujihesabia haki ili kutafuta haki ya Mungu, ambayo alikuwa amekuja kuitimiza. Bila shaka, neno hili kutimiza hapa linahitaji ufafanuzi fulani. Wakati mwingine linafikiriwa kimakosa kwamba siku zote lina maana ya kutokea kwa jambo fulani lililotabiriwa, lakini uchunguzi wa matumizi yake katika Agano Jipya, na hasa katika Mathayo, hautoi maana hii inayodhaniwa katika hali zote. Kwa lugha rahisi kutimiza kunaweza kumaanisha (1) kujaza au kujaliza (taz. Yh 15:11; Lk 2:40); au (2) kukamilisha, kutimiliza (taz. Yh 7:8, 30); au (3) kutambua, kufanyia kazi, kutekeleza (rej. Gal. 5:14; Rum. 13:8). Maana ya tatu inaonekana kuwa ndiyo mantiki hasa ya madai ya Kristo kuhusu kutimiza (yaani, kutambua, kutekeleza) Agano la Kale. Yaani, sheria za maadili za Agano la Kale zinatambuliwa na kutekelezwa katika maisha na mafundisho ya Kristo. Kielelezo kutoka katika Nukuu za Agano la Kale Ni muhimu kutambua katika suala hili kwamba kuna vifungu dhahiri katika Mathayo ambapo neno “timiliza” halimaanishi kutimia kwa kile kilichotabiriwa hapo awali . Utimilifu umetumika mara kumi na tano kuhusiana na Kristo katika Mathayo (1:22; 2:15, 17, 23; 3:15; 4:14; 5:17;
49
Made with FlippingBook Digital Publishing Software