Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
8:17; 12:17; 13:35; 21:4; 26:54, 56; 27:9, 35). Kati ya vifungu hivi, kadhaa vinathibitisha kwa uwazi nadharia kwamba vifungu vya Agano la Kale vinavyohusianishwa na Kristo havikuwa vyote vya kiunabii hasa hasa, lakini kulikuwa na kanuni fulani katika vifungu husika ambazo zilitimizwa au kukamilishwa katika Kristo. Usomaji wa Hosea 11:1 katika muktadha wake unatoa maana kwamba wito wa Mungu kwa “Mwanawe kutoka Misri” unarejelea ukombozi wa taifa wakati lilipotoka Misri (Kut. 4:22). Na bado kifungu hiki kinatumika kuhusiana na kurudi kwa Mtoto Yesu kutoka Misri kwa kutumia maneno: “Ili litimie ” (Mt. 2:15). Ni dhahiri vya kutosha kwamba Hosea 11:1 haikutabiri moja kwa moja kurudi kwa Yesu kutoka Misri, na bado tukio hili linarejelewa kama utimilifu wa mstari huo wa Agano la Kale. Hakika ni utimilifu wa yale aliyosema Hosea ikiwa utimilifu unamaanisha kutambua kanuni ya msingi inayohusika katika kifungu hicho, yaani, utume wa Kimasihi wa Israeli. Kwa maana, sababu ya Mungu kuwaita kutoka Misri na kuingia katika nchi takatifu ilikuwa ni kwa ajili ya kumzaa Mtoto mtakatifu Yesu, ambaye angewaokoa na dhambi zao (rej. Mwa. 12:1 pamoja na Mt. 1:21). Kwa maana hii taifa la Kimasihi linajitimiliza lenyewe tu katika kutekeleza utume wa Kimasihi, ambao ulikuwa ni kumzaa Masihi. Hapa Hosea hakutabiri juu ya Kristo, lakini Kristo alitimiza yale ambayo Hosea alisema kwa kuwa alitekeleza na kutambua kupitia maisha yake, kwa njia kamilifu zaidi, kile kinachomaanishwa na “mwanangu” na “kuitwa kutoka Misri.” Inaweza kutolewa hoja kinzani kwamba katika maana hii pana ya neno kutimiza karibu kila kitu katika Agano la Kale kinaweza kutumika kwa kuhusianishwa na Kristo. Kwa kweli, inaonekana kuwa huo ndio ukweli hasa. Kwa hakika, hii inadhihirisha kikamilifu kile kinachodokezwa katika madai ya Yesu kwamba Agano la Kale lote “limetimizwa” ndani Yake (Mt. 5:17). Mtu hangeshuku, kwa mfano, kwamba Yeremia 31:15 ilimaanisha
50
Made with FlippingBook Digital Publishing Software