Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

chochote zaidi ya maombolezo ya Raheli kwa ajili ya utumwa wa watoto wake kule Babeli, lakini Mathayo anasema hili “limetimizwa” kupitia mauaji ya watoto wasio na hatia waliouawa na Herode (Mt. 2:18). Wala, mtu hangeweza kukisia kutokana Isaya 11:1 pekee kwamba, anaporejelea Kristo kama “tawi” ( Nezer ), kwamba huu ulikuwa unabii wa kwamba angeishi Nazareti (“mji wa vichaka”) (Ona Lange’s Commentary on the Holy Scriptures . Grand Rapids: Zondervan, n. d. kuhusu Mt 2:23) au maoni mengine kuhusiana na mstari huu (Ona Geisler, The Big book of Bible Difficulties , Baker, 2008). Vivyo hivyo, haionekani wazi katika Zaburi 78:2 kwamba Asafu anazungumza juu ya mbinu ya Kristo ya kufundisha kwa njia ya mifano alipoandika, kama anavyonukuliwa na Mathayo, “Nitafumbua kinywa changu kwa mifano, Nitayatamka yaliyositirika tangu awali” (Mt. 13:35), wala kwamba Zekaria (Zek. 11:12-13, taz. Yer. 32:6, 8) alimaanisha kutabiri kiasi cha pesa za usaliti aliporejelea ujira wake kutoka kwa wafanyabiashara wa kondoo (Mt. 26:15). Lakini katika hali hizi zote kuna kanuni inayohusika, iwe ya Kimasihi au ya kimaadili, ambayo inatimizwa au kufikia ukamilifu katika maisha ya Kristo. Ni katika maana hii pana ya neno utimilifu ndipo Yesu anajirejelea mwenyewe kama utimilifu wa haki ya Agano la Kale katika Mathayo 5:17. Kristo “alizaliwa chini ya sheria” (Gal. 4:4), katika mafundisho yake alifafanua maana ya kweli na ya ndani ya Torati, na akatoa kielelezo cha namna ya kuishika kikamilifu kupitia maisha yake. Yesu alionyesha kwamba kiini cha Sheria ni upendo (Mt. 5:43, rej. 22:37-40), na upendo ndio alioutekeleza kikamilifu zaidi (taz. Yh. 15:13). Kile ambacho Sheria ilidai, ni Kristo peke yake alikitoa; kwa hiyo, Agano la Kale lote lilikuwa ni maandalizi ya ukamilifu na utimilifu ambao Kristo aliudhihirisha katika maisha yake.

51

Made with FlippingBook Digital Publishing Software