Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

Mafundisho ya Kristo ni Utimilifu wa Agano la Kale Mengi ya yale ambayo yamesemwa hadi sasa yanahusu maisha ya Kristo kama utimilifu au ukamilifu wa sheria za maadili za Agano la Kale. Hata hivyo, mafundisho ya Kristo yanapaswa kujumuishwa katika kile kinachomaanishwa na kuja kwake ili kutimiza Agano la Kale. Pengine jambo hili linaonekana vyema kwa kuutazama muktadha wa karibu wa Mathayo 5:17, ambapo Yesu anatofautisha tafsiri yake ya Agano la Kale na mapokeo potofu ya siku zake. “Mmesikia kwamba imenenwa... lakini mimi nawaambia” (5:21-22, 27-28, 21-32, 33-34, 38-39, 43-44), Yesu alirudia kauli hii mara sita. Katika kila moja ya uthibitisho huu mkuu Kristo anatofautisha roho au kiini cha Torati (ambayo aliithibitisha) dhidi ya andiko la Torati (ambalo Wayahudi walifundisha). Mafundisho yake yalikwenda kwenye moyo wa Agano la Kale na kuufunua moyo wa Agano la Kale. Kwa upande mwingine, Mafarisayo walikuwa wameficha au kuharibu maana halisi ya Maandiko. Ikumbukwe kwamba Yesu anarejelea tafsiri yao potofu kwa maneno “mmesikia” na sio “imeandikwa.” Kristo anaposema, “Lakini mimi nawaambia,” anathibitisha maana ya kweli ya Agano la Kale. Au kwa lugha bora zaidi, Kristo “anafunua” au “anajaliza” maana ya kweli ambayo Agano la Kale liliibeba. Walikuwa “wamesikia” kwamba kitendo cha kuua kilikuwa kibaya, lakini Yesu alifundisha kile ambacho kilimaanishwa hasa katika kile “kilichoandikwa,” yaani, kwamba hata wazo la kuua (chuki) lilikuwa baya (Mt. 5:21-22). Tena, walikuwa “wamesikia” kwamba tendo la uzinzi lilikuwa kosa, lakini Yesu anaonyesha kwamba maana ya kweli ya amri hii ilimaanisha kwamba hata nia ya tamaa ni mbaya. Na katika kifungu cha mwisho, sehemu ya yale “yaliyosemwa” ya zamani haimo hata katika Agano la Kale, achilia mbali kufasiriwa vibaya. Sehemu ya “Mpende jirani yako” kwa kweli imo, lakini “na, Umchukie adui yako” haimo (5:43). Badala

52

Made with FlippingBook Digital Publishing Software