Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

yake, kinachodokezwa katika Agano la Kale kwa hakika ni “Wapende adui zako” (rej. Mithali 24:17). Huu ni ufafanuzi wa mafundisho haya ya siri ya Agano la Kale ambayo yanatimizwa au “kukamilika” katika mafundisho ya Kristo. KRISTO: UTIMILIFU WA AHADI ZA WOKOVU Kuna kifungu kimoja zaidi, Yohana 5:39-40, ambamo Kristo anadai kuwa Yeye ndiye ujumbe wa Agano lote la Kale. Aliwaambia Wayahudi, “Mwayachunguza [kweli] maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake [si kupitia hayo]; na hayo [Maandiko] ndiyo yanayonishuhudia. Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima [ambao mnajifanya kuwa mnautafua].” J. B. Phillips anatafsiri hivi, “Mnachunguza maandiko, kwa kuwa mnafikiri kwamba mtapata uzima wa milele ndani yake. Na wakati wote yananishuhudia mimi! Lakini hamko tayari kuja kwangu kupokea uzima halisi!” Maana ya wazi ya kifungu hiki lazima ipatikane ndani ya muktadha wake. Lilikuwa ni onyo dhidi ya kutafuta uzima wa milele katika Maandiko, kana kwamba yana uzima ndani yake peke yake, badala ya kupata uzima wa milele katika Kristo kupitia Maandiko. Usomaji wa Biblia kama huo (ibada ya Biblia) kwa kweli uliwapeleka mbali na Kristo badala ya kuwaongoza kwa Kristo. Walijua ganda la Biblia lakini walikuwa wakipuuza kokwa ndani yake. Sio Kitabu kinachookoa, bali ni Mwokozi wa Kitabu. Hii ni aina ya njia ya nne ambayo Kristo anaweza kuonekana katika Agano la Kale, yaani, kama utimilifu wa ahadi zake za wokovu . Hii ni tofauti kwa kiasi fulani na mbinu zile nyingine tatu za ufasiri wa A.K katika msingi Kristo: (1) Unabii wa Kimasihi unamwonyesha Kristo kama Masihi na Mfalme; (2) mfumo wa ukuhani wa Walawi unamdhihirisha Yesu kama Kuhani na Dhabihu, na (3) sheria za maadili zinamfunua kama Nabii na

53

Made with FlippingBook Digital Publishing Software