Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

Mwalimu mkuu. Lakini, (4) mtazamo wa Kristo kama utimilifu wa ahadi za kiroho za Agano la Kale unamtambulisha kama Mwokozi na Bwana. Kiwango ambacho Agano la Kale linatoa tumaini la wokovu na uzima wa milele, ndicho kiwango icho hicho ambacho linazungumza juu ya Kristo. Zaidi ya hayo, kiwango ambacho Agano la Kale linazungumza juu ya Kristo, ndicho kiwango ambacho pia linatoa uzima wa milele. Injili ya Yohana yenyewe ni kielelezo cha mtazamo huu wa Kikristo kwa Agano la Kale. Kristo ndiye Mpaji wa Uhai na Mwokozi katika Maandiko yote ya Agano la Kale. Sasa madai hayo ni sawa na kujitambulisha kama Mungu, kwa maana katika Agano la Kale ni Mungu pekee ndiye anayeokoa. “Mimi, naam, mimi, ni Bwana, zaidi yangu mimi hapana mwokozi” (Isa. 43:11). Lakini Yohana aliandika juu ya Kristo: “… tena twajua ya kuwa hakika huyu ndiye Mwokozi wa ulimwengu” (Yh 4:42). Sasa tafsiri kama hiyo ya “Kikristo” ya Maandiko ya Kiyahudi, ambayo inamhusianisha Yesu Kristo na vifungu vyote vinavyozungumzia wokovu katika Agano la Kale, kwa vyovyote ingetarajiwa kuamsha uadui na chuki fulani upande wa Wayahudi ambao wanaamini katika Mungu mmoja, na ndivyo ilivyokuwa. Yesu alisema, “Mimi na Baba tu umoja.” Kisha, “Wayahudi wakaokota mawe tena ili wampige,” jambo ambalo walisema walitaka kulifanya sababu yao ikiwa ni “kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu” (Yh 10:30-31, 33) . Katika tukio lililotangulia, Yesu alikuwa amemwita Mungu “Baba” yake, “Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa…. alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu.” (Yh 5:18). Hakukuwa na shaka akilini mwa Wayahudi kuhusu kile ambacho Yesu alimaanisha katika madai yake. Aliposema, “Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko ,” wao tena “wakaokota mawe ili wamtupie” (Yh 8:58-59). Walimwelewa kuwa alijehesabia kuwa mwenye

54

Made with FlippingBook Digital Publishing Software