Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

wangu sitampa mwingine.” Na bado Yesu alishiriki utukufu huu hata kabla ya ulimwengu kuwako (Yh 17:5), na Yohana anasema kwamba ulikuwa ni utukufu wa Yesu ambao Isaya aliuzungumzia (Yh 12:41). Ingawa aina hii ya kulitazama Aganao la Kale katika msingi wa Kristo ndiyo inayotawala Injili ya Yohana na Ufunuo, haipatikani katika vitabu hivi pekee. Katika jedwali inayofuata hapa chini kuna maandiko mengine ya ziada yaliyochaguliwa ambayo yanaonyesha kwamba Yesu ni Yehova, yaani, Mungu wa Agano la Kale. Rejea ya mwisho ni tamko lenye nguvu sana la uungu wa Kristo. Katika Isaya 45, Yehova anena, akisema: “maana mimi ni Mungu; hapana mwingine. Kwa nafsi yangu nimeapa…. ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa” (Isa. 45:22-23). Maneno haya haya yananenwa kwa habari ya Kristo: “ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana [ Yehova , katika chuo cha Isaya], kwa utukufu wa Mungu Baba.” (Flp. 2:10). Yesu ni Yehova, na siku moja kila nafsi itakiri hilo. Yehova (Mungu) Cheo au Tendo la Pamoja Yesu Zab. 18:2 Mwamba 1 Kor. 10:4 Yer. 31:34 Msamaha wa dhambi Mk 2:7, 10 Zab. 148:2 Aliabudiwa na Malaika Ebr. 1:6 Kote katika A.K Maombi kumwelekea Mdo 7:59 Zab. 148:5 Muumbaji wa Malaika Kol. 1:16 Isa. 45:23 Ukiri kama Bwana Flp. 2:10 Sambamba na kumwona Bwana na Mwokozi wa Agano la Kale kuwa ni Yesu, kama ambavyo Yohana 5:39 inaonekana kudokeza, tunaona pia kuwa utambulisho wa “malaika wa BWANA (Yehova)” ni Yesu Kristo.

56

Made with FlippingBook Digital Publishing Software