Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

25:8), hata hivyo, kitabu chake ndicho kinachoanza sehemu ya Agano la Kale ambayo ni tofauti na “Torati ya Musa” na inaitwa “Manabii.” Tofauti hii kati ya “Musa” na “Manabii” inaonekana hata katika nyakati za Agano la Kale. Mapema sana wakati wa utumwa (karne ya sita, K.K), Danieli alirejelea “Torati ya Musa” (9:11, 13) na “vitabu” (9:2), ambavyo kati yake kulikuwa na “neno la BWANA kwa Yeremia nabii” (9:2). Hii inaweza kuonekana kuashiria kwamba “Musa” na “Manabii” waliwekwa katika makundi mawili tofauti. Katika kipindi cha baada ya utumwa (karne ya tano, K.K), Zekaria anazungumza kuhusu watu wakaidi ambao “walifanya mioyo yao kuwa kama jiwe gumu, wasije wakaisikia sheria na maneno ya Bwana wa majeshi, aliyoyapeleka kwa roho yake kwa mkono wa manabii wa kwanza ” (7:12, taz. 1:4; 7:7). Katika Ezra 9:11 neno “manabii” limetumika kujumuisha Musa (rej. Kum. 18:15) na manabii wengine baada yake, kama ambavyo neno Torati wakati mwingine linatumiwa kujumuisha maandiko ya manabii na Musa kadhalika. Nehemia (9:26) anatoa tofauti kama hiyo, anaposema “...hawakukutii, wakakuasi, wakaitupa sheria yako nyuma yao, wakawaua manabii wako...” (taz.9:30). Mgawanyo huu huu wa “Torati na Manabii” uliendelea katika kipindi cha kati ya A.K na A.J, kwa mfano, katika Mwongozo wa Nidhamu wa Bahari ya Chumvi (I, 3; VIII, 15) na katika fasihi ya kidini ya maagano (taz. 2 Mak. 15:9). Katika Agano Jipya, mgawanyo wa sehemu mbili za “Torati na Manabii” ni mojawapo ya njia za kawaida za kurejelea Agano la Kale. Unatokea mara kumi na mbili (rej. Mt. 5:17; 7:12; Lk 24:27). Katika kifungu hiki cha mwisho neno “Torati na Manabii” linafafanuliwa kama “maandiko yote” na, katika Luka 16:16, kama kila kitu kilichovuviwa na Mungu, kuanzia kwa Musa hadi Yohana Mbatizaji.

80

Made with FlippingBook Digital Publishing Software