Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

Sehemu Mbili za Agano Jipya

Injili Nne Kama ambavyo Agano la Kale linatazamwa kama Torati na Manabii, Agano Jipya linaweza kugawanywa vivyo hivyo katika Injili na Nyaraka, huku Matendo na Ufunuo zikijumuishwa katika fungu la mwisho. Katika mpangilio wa vitabu vya Agano Jipya, Injili nne kwa kawaida zinasimama kwanza, kwa sababu zinaelezea maisha, mafundisho, kifo na ufufuo wa Kristo, mambo ambayo yaliunda msingi wa kanisa, ambao Nyaraka zinauzungumzia baadaye. Nyaraka Sehemu nyingine ya Agano Jipya inahusiana na Injili kwa namna ile ile mitume walivyokuwa na uhusiano na Kristo. Injili zinaandika kile Yesu alichofundisha, na Nyaraka zinaandika kile ambacho mitume walifundisha juu yake. Katika mwelekeo huu basi, Agano la Kale limegawanywa katika Musa na Manabii na Agano Jipya katika Kristo na “Mitume.” Na ili kukuza uhusiano huu, inaweza kuzingatiwa kuwa Nyaraka kwa Injili ni kama Manabii walivyokuwa kwa Torati. Kwa lugha nyingine, Nyaraka ni kama jengo lililojengwa juu ya msingi wa Injili, kama ambavyo Manabii walijenga juu ya msingi wa Torati. Kristo Katika Sehemu Nne za Biblia Kwa kuwa Kristo amethibitika kuwa mada kuu ya Biblia nzima (ona sura ya 2-3), ukweli unaofuata ni kwamba Yeye ndiye mada ya kila sehemu ya Biblia. Kwa kweli, kwa kuwa Kristo ndiye kiunganishi anayefanya sehemu zote za Maandiko kuwa moja, basi vyovyote ambavyo Biblia inaweza kugawanywa, mtu lazima atafute kuangazia namna sehemu za mgawanyo husika zinavyoelekeza kwenye mada ya msingi ambayo ni Kristo. Ikiwa mgawanyo wa sehemu nne utafuatwa, basi Kristo anaweza

81

Made with FlippingBook Digital Publishing Software