Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

kuonekana kama mada inayoendelea kujifunua, ambayo inaunganisha Biblia nzima pamoja kwa njia ifuatayo: Mada Moja Mgawanyo katika Sehemu Mbili Mgawanyo katika Sehemu Nne

Torati—Msingi kwa ajili ya Kristo Unabii—Matarajio ya Ujio wa Kristo Injili—Kudhihirishwa kwa Kristo Nyaraka—Ufafanuzi juu ya Kristo

Taraja la Ujio wa Kristo (A.K) Kutokea kwa Kristo (A.J)

Kristo

Torati: Msingi kwa ajili ya Kristo Kama alivyo Musa na Torati yake kwa Agano la Kale ndivyo alivyo Kristo na Injili yake kwa Agano Jipya, yaani, msingi wa yote yanayofuata. Kimsingi, Biblia inamlinganisha Musa na Kristo katika njia kadhaa za msingi katika mantiki hii. Kwanza, Yohana anasema, “Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.” (Yh 1:17). Sasa kama vile Torati ya Musa ilivyokuwa msingi kwa ujumbe wa manabii waliomfuata, ndivyo hivyo neema na kweli ya Injili ya Kristo ilivyo msingi wa ujumbe wa mitume. Zaidi ya hayo, wote wawili Musa na Kristo walikuwa wapatanishi wa maagano yao; Musa alikuwa mpatanishi wa agano la kale na Kristo ndiye mpatanishi wa agano jipya (Ebr. 8:6; Gal. 3:19). Waisraeli, ambao walitolewa utumwani kwa mkono wa Musa, wanasemekana kuwa “walibatizwa wawe wa Musa” (1 Kor. 10:2), kama ambavyo Wakristo “wamebatizwa katika Kristo” (Rum. 6:3). Hatimaye, wote wawili walishiriki mng’ao wa utukufu wa Mungu (2 Kor. 3:7; Yh. 1:14). Nafasi ya Musa na Sheria yake katika Agano la Kale ilikuwa ya msingi kwa kile kilichofuata katika Agano hilo, kama ambavyo kile Kristo alichofundisha katika Agano Jipya kilikuwa msingi wa kweli ya Agano Jipya.

82

Made with FlippingBook Digital Publishing Software