Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

Torati ya Musa iliweka msingi kwa ajili ya Kristo kwa njia kadhaa: • Kwa njia ya kivuli , Torati ya Musa iliweka vivuli na mifumo ya msingi ambayo baadaye ilitimizwa katika Kristo (ona sura ya 2). • Kwa njia ya maandalizi ya kimaadili , Torati ya Musa iliwafunza wanadamu katika misingi ya mema na mabaya hadi pale hatia yao ilipowaongoza kwa Kristo ili wapate msamaha (taz. Gal. 3:19-24; Rum. 3:19-22). • Kwa njia ya unabii , Torati ya Musa iliandika tumaini la kwanza na la msingi la Kimasihi kwa watu wa Israeli (rej. Mwa. 3:15; 49:10; Kum. 18:15). Unabii: Matarajio ya Ujio wa Kristo Kwa kuwa Torati ya Musa ilikuwa imeweka msingi kwa ajili ya Kristo katika njia hizi tatu za msingi, ilikuwa kawaida kwamba wale waliokuja baada yake wangetazamia kwa hamu kutimizwa kwa matumaini hayo. Musa alikuwa amewaahidi Waisraeli, “Bwana, Mungu wako, atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye” (Kum. 18:15). Na maandiko yote baada ya Musa, kwa njia moja au nyingine, yalikuza matarajio haya. Katika Yoshua tumaini lilikuwa kubwa tangu watu walipoimiliki nchi ambayo Mungu alikuwa amewaahidi katika kujitayarisha kwa ajili ya utume wao wa Kimasihi. Katika Waamuzi kulikuwa na wakombozi wengi na waokozi (kama Gideoni, Baraka, Samsoni), lakini Mwokozi hakutokea. Samweli aliweka tumaini kwa uwazi zaidi katika kuanzishwa kwa ufalme, upako wa Mfalme Daudi, ambaye kupitia kwake “Mpakwa mafuta” (Masihi) aliahidiwa kuja (2 Sam. 7:12-). Mwanzoni mwa Wafalme matarajio ya Kimasihi yalikuwa kwenye kilele, lakini punde baadaye yalipungua kwa sababu ya mitala, ibada ya sanamu na mgawanyiko wa mwisho wa ufalme mkuu wa Sulemani. Ufalme wa Israeli ilipozidi

83

Made with FlippingBook Digital Publishing Software