Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
kuzorota, manabii (Isaya, Yeremia, Ezekieli, Danieli na wale Kumi na Wawili) waliendeleza moto wa matarajio ya Kimasihi hadi sura ya mwisho kabisa ya Agano la Kale (Mal. 4:2). Matarajio yao yalitiwa mkazo na kurudi kwa Yuda kutoka utumwani Babiloni, kama ilivyoandikwa katika Ezra, na ujenzi wa taifa unaosimuliwa katika Nehemia. Bila shaka, washairi wa Israeli pia walikuwa wameongeza tumaini hili kwa matarajio yao mengi ya kiroho na, wakati fulani, hata utabiri wa Kimasihi. Injili: Kudhihirishwa kwa Kristo Ni Nabii Isaya, katika kumtazamia Kristo, aliyesema kwamba Masihi angetambulishwa kwa “sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana” (Mt. 3:3, kutoka Isa. 40:3). Na Agano Jipya linapofungua pazia lake, hivyo ndivyo Yohana Mbatizaji anavyofanya. Yohana anapoulizwa kwa nini anamtangaza Kristo, anajibu: “kusudi [Kristo] adhihirishwe kwa Israeli” (Yh 1:31). Kwa maneno mengine, Yule ambaye Musa alimwekea msingi na ambaye manabii walimtazamia amekuja katika udhihirisho wa kihistoria, katika mwili halisi. Katika Kristo matarajio ya Agano la Kale yanakuwa utimilifu ndani ya Agano Jipya. Unabii unakuwa historia, kwa sababu Logos (Kristo) amekuja katika cosmos, yaani ulimwengu (Yh 1:14). Kwa nini udhihirisho huu wa Kristo ulimwenguni? Agano Jipya linatoa majibu mengi muhimu kwa swali hili. 1. Petro anasema Kristo “ alifunuliwa mwisho wa zamani…. hata imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu” (1 Pet. 1:20-21). 2. Yohana aliandika “ya kuwa yeye alidhihirishwa , ili aziondoe dhambi “ (1 Yh 3:5), na 3. “Kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa , ili azivunje kazi za Ibilisi” (1 Yh 3:8), au
84
Made with FlippingBook Digital Publishing Software