Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
4. Ili kuonyesha kwamba “pendo la Mungu lilionekana kwetu…. ili tupate uzima kwa yeye” (1 Yh 4:9). 5. Paulo anasema Kristo alikuja kuwadhihirishia watakatifu wake “…siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote…” (Kol. 1:26). 6. Mahali pengine, Paulo anaandika juu ya wokovu na wito wa mwamini, ambao sasa “… unadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu” (2 Tim. 1:9-10). 7. Yesu, akiomba kwa Baba yake, alieleza kusudi la kutokea kwake kwa maneno haya: “Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu” (Yh 17:6). Kristo alidhihirishwa mara ya kwanza kwa ulimwengu, “wala ulimwengu haukumtambua. Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea” (Yh 1:10-11). Hii ndiyo sababu alijidhihirisha kwa wanafunzi wake na “Wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake” (Yh 1:12). Nyaraka (na Matendo): Tafsiri ya Kristo Agano la Kale linaweka msingi kwa ajili ya ujio wa Kristo na kumtazamia kwa matarajio makubwa. Agano Jipya linatoa udhihirisho wa kihistoria wa Kristo katika Injili. Katika Nyaraka, mitume wanatoa tafsiri rasmi ya kudhihirishwa kwa Kristo na maana yake kwa maisha ya waamini. Yesu aliwafundisha mitume wake kwa miaka mitatu na nusu kabla ya kifo chake na kisha kwa siku arobaini baada ya kufufuka kwake (Mdo 1:3), lakini Yeye mwenyewe hakuandika tafsiri yoyote ya utume wake. Yesu aliwaachia kazi hii mitume wake, akiwapa na ahadi hii: “Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina
85
Made with FlippingBook Digital Publishing Software