Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia” (Yh 14 :26). Nyaraka ishirini na mbili za Agano Jipya zilikuja kama utimilifu wa ahadi hiyo. Nyaraka hizo ni kumbukumbu ya tafsiri ya mitume kuhusu udhihirisho wa Yesu Kristo katika ulimwengu huu. Kabla mitume hawajaandika tafsiri yao ya kimamlaka ya mafundisho ya Kristo, kifo, ufufuo na kupaa kwake, Kanisa la kwanza liliongozwa na huduma zao zilizo hai: (1) Kanisa, tangu lile la kwanza kabisa walikuwa “wakidumu katika fundisho la mitume” (Mdo. 2:42), (2) Hata kwa “kuwekewa mikono ya mitume waamini walipewa Roho Mtakatifu” (Mdo 8:18, RSUVDC), (3) Masuala makuu ya kanisa yaliamuliwa kwa matamko ya mitume (Mdo. 15:22), (4) Kanisa lilihimizwa “mkayashike mapokeo mliyofundishwa” na mitume (2 Thes. 2:15), au (5) kukumbuka “amri ya Bwana na Mwokozi iliyoletwa na mitume wenu” (2 Petro 3:2). Mara huduma hai ya mitume ilipokoma, tafsiri pekee yenye mamlaka ya Kristo ilikuwa ni maandiko ya mitume ya Agano Jipya. Hata kabla ya mtume wa mwisho (Yohana) kufa, kulikuwa na mkusanyo unaokua wa maandiko yao, ambayo yalizingatiwa na Kanisa kuwa tafsiri yenye mamlaka ya ujumbe wa Kristo. Petro anaeleza juu ya mkusanyo wa barua za Paulo, alizozijumuisha pamoja na “maandiko mengine” (2 Pet. 3:15 16). Maandiko ya Paulo yalikuwa yakisomwa na kusambazwa miongoni mwa makanisa (Kol. 4:16). Yuda, mojawapo ya vitabu vya baadaye vya Agano Jipya (ambacho pengine kiliandikwa baada ya Paulo na Petro kuuawa kishahidi), ananukuu barua ya Mtume Petro (Yuda 17-18). Hatua kwa hatua tafsiri iliyoandikwa ilichukuwa nafasi ya tafsiri hai ya Agano Jipya. Hii haimaanishi kwamba kumbukumbu iliyoandikwa sasa ilianza kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu: “Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu” (2 Pet. 1:20-21). Kwa lugha nyingine, hii ni tafsiri ya ujumbe wa Kristo kutokana na nuru ya

86

Made with FlippingBook Digital Publishing Software