Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
Roho wa Mungu kupitia Neno la Mungu. Kristo alisema, “Maandiko ... yananishuhudia,” na “Roho ... atawaongoza awatie kwenye kweli yote” (Yh 5:39; 16:13).
KRISTO KAMA MSINGI: MGAWANYO WA MAANDIKO KATIKA SEHEMU SITA
Msingi wa Mgawanyo wa Biblia katika Sehemu Sita Uchambuzi uliotangulia unaonyesha jinsi Kristo anavyoweza kuhusishwa na Maandiko yanapogawanywa katika sehemu nne. Hata hivyo, tangu zamani sana, Wayahudi waligawanya Agano lao la Kale katika sehemu tatu (baadaye ziliitwa Torati, Manabii, Maandiko); na kwa ulinganifu huo Agano Jipya linaweza kupewa mgawanyo wa sehemu tatu, ukizingatia kitabu cha Matendo kuwa tofauti na Nyaraka, hivyo kutoa sehemu sita za Biblia nzima. Mapema takriban mwaka 200 K.K. Agano la Kale la Kiebrania wakati fulani liligawanywa katika “Torati na Manabii na vitabu vingine” (Dibaji ya Ecclesiasticus [Sira]). Hatuambiwi ni vitabu gani vilikuwa katika fungu gani, ila tu vilijumuisha “mafundisho mengi makuu” kuhusu Israeli. Josephus (37—100 B.K) anafafanua kwa namna mahususi zaidi katika mgawanyo wake wa sehemu tatu za Agano la Kale. Anasema kulikuwa na vitabu vitano vya Musa, manabii kumi na watatu, na “vitabu vinne vyenye nyimbo za Mungu” ( Against Apion , I, 8). Hata hivyo, ushuhuda wa kwanza kabisa wa mgawanyo wa sasa wa Kiebrania wa sehemu tatu za Agano la Kale unatokana na Talmud ya Babeli, ambayo katika hali yake ya sasa inakadiriwa kuwepo tangu karne ya tano B.K. Inaorodhesha vitabu hivyo kwa idadi ya ishirini na vinne na kuvigawa katika sehemu hizi tatu:
87
Made with FlippingBook Digital Publishing Software