Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

I. Torati—5 • Mwanzo—Kumbukumbu la Torati II. Unabii—8

• Manabii wa Kale—Yoshua, Waamuzi, Samweli, Wafalme • Manabii wa Mwisho—Isaya, Yeremia, Ezekieli, Kumi na Wawili (wadogo) III. Maandiko - 11 • Washairi—Zaburi, Mithali, Ayubu • Vitabu—Wimbo wa Sulemani, Ruthu, Maombolezo, Esta, Mhubiri • Historia—Danieli, Ezra-Nehemia, Mambo ya Nyakati Mgawanyo wa sehemu mbili za Agano la Kale ulikuwa na Torati na Manabii pekee, kwani kila mtu aliyeandika baada ya Musa alipaswa kuwa “nabii” kwa maana ya kwamba alikuwa mmoja wa watu ambao Mungu alinena kupitia kwao. Kwa maana hii ya neno nabii , hata Daudi (Mdo 2:30) na Sulemani (1 Falm 4:29; 3:11) walikuwa manabii, waandishi wote wa Agano la Kale, akiwemo Musa, waliitwa manabii (taz. Ezra 9:11; 1 Pet. 1:20). Lakini kwa vile Musa alikuwa mkombozi, mtoa-sheria mkuu na nabii, vitabu vyake viliwekwa katika fungu la peke yake, na wengine waliitwa “Manabii.” Haijawekwa bayana ni kwa nini au ni lini “Manabii” waliwekwa kwa mara ya kwanza kwenye fungu moja kama “manabii na vitabu vingine” au “manabii na vitabu vyenye nyimbo za Mungu.” Yafuatayo ni maoni kadhaa ambayo yametolewa: • Vitabu vya fungu la tatu havikuzingatiwa kuwa na mamlaka sawa na “Torati na Manabii” na hivyo viliwekwa katika kundi tofauti.

88

Made with FlippingBook Digital Publishing Software