Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

• Sehemu ya mwisho ilikuwa ya mwisho kuandikwa na kukubalika katika kanoni na kwa sababu hiyo inakaa mwishoni mwa Agano la Kale. • Vitabu hivyo vilivyoandikwa na watu waliokuwa na karama ya unabii tu lakini hawakuwa na cheo au ofisi ya kinabii viliwekwa katika tabaka la tatu peke yake. • Vitabu vya sehemu ya tatu viliwekwa hapo kwa sababu ya mada zake au matumzi ya sikukuu (kutumika kwa ajili ya sikukuu na karamu mbalimbali). Kwa ujumla, sababu mbili za kwanza zinaungwa mkono na wasomi huria na mbili za mwisho zinashikiliwa na wanazuoni wa kihafidhina. Kwa msingi wa mamlaka ya Yesu (rej. sura ya 1), ambao unaungwa mkono na Josephus, mitazamo miwili ya kwanza haikubaliki. Kwa mfano, kitabu cha Danieli, ambacho kimewekwa katika “maandiko” hakikuandikwa kwa kuchelewa (k.m., karne ya pili, K.K.) kwa sababu kinajifafanua kuwa ni utabiri wa matukio ya kabla ya wakati huo (taz. sura ya 2, 7). Yesu alisema Danieli alikuwa “nabii” (Mt. 24:15), na inaonekana Josephus alimworodhesha Danieli miongoni mwa manabii, kwa sababu Danieli kwa hakika si “wimbo.” Pia kuna uthibitisho mzuri wa ndani kwamba kitabu cha Ayubu na zaburi nyingi ziliandikwa mapema sana. Kristo ndani ya Mgawanyo wenye Sehemu Sita Haijalishi ni sababu gani ya kweli iliyofanya Agano la Kale kuwa na mgawanyo wenye sehemu tatu, kuna dalili kwamba Yesu Mwenyewe alitambua mgawanyo huo wakati mmoja (Luka 24:44). Inafikiriwa kuwa Yesu, kwa kule kurejelea Torati, Manabii na Zaburi, alithibitisha kuwepo kwa mgawanyo wa sehemu tatu za Agano la Kale. Zaburi, kwa kuwa ndicho kitabu cha kwanza na kikubwa zaidi cha sehemu hiyo, kinachukuliwa kama utambulisho wa sehemu nzima.

89

Made with FlippingBook Digital Publishing Software