Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

La muhimu si jinsi Biblia inavyogawanywa bali jinsi inavyohusiana. Ikiwa kuna sehemu tatu, basi sehemu zote tatu lazima ziwe na uhusiano na Kristo. Hilo laweza kufanywa kwa njia iliyoonyeshwa katika jedwali inayofuata hapa chini. Mgawanyo wenye Sehemu Nne Mgawanyo wenye Sehemu Sita Torati—Msingi kwa ajili ya Kristo Torati—Msingi kwa ajili ya Kristo Unabii—Matarajio ya Ujio wa Kristo Unabii—Matarajio ya Ujio wa Kristo Maandiko—Matamanio ya Ujio wa Kristo Matamanio na Matarajio ya Ujio wa Kristo Uchambuzi wa jedwali unafunua ukweli kwamba muundo wa sehemu sita unahusisha tu kugawanya “Manabii” katika “Manabii” na “Maandiko.” Mgawanyo huu unafaa zaidi kwa maana ya muundo wenye msingi wa Kristo kwa sababu unatenganisha mashairi (Maandiko) na unabii, fungu la pili—kama kawaida ya mwelekeo wa washairi— likisisitiza matamanio ya ujio wa Kristo, na fungu la kwanza—kama manabii wanavyopaswa kufanya—linasisitiza matarajio ya Kristo. Kama ilivyo kwa mgawanyo mwingine wowote, mgawanyo huu hauna usahihi wa asilimia mia moja kwa vile kuna ushairi katika Manabii (rej. Isaya), na unabii katika maeneo kadhaa ya vitabu vya mashairi (taz. Zab. 2, 16, 22). Vyoyote iwavyo, mgawanyo wa Agano la Kale katika sehemu tatu unaleta maana ya jumla katika mantiki ya kuzingatia mada ya ujio wa Kristo. Kwa kweli, zikichukuliwa pamoja na Torati, zinawasilisha matarajio ya pande tatu kuhusu Kristo katika Agano la Kale. Injili—Kudhihirishwa kwa Kristo Injili—Kudhihirishwa kwa Kristo Matendo—Uenezi wa Kristo Nyaraka—Ufafanuzi juu ya Kristo Nyaraka—Ufafanuzi juu ya Kristo

90

Made with FlippingBook Digital Publishing Software