Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

Katika Torati kuna mtazamo wa kushuka chini kwa namna msingi unavyowekwa kwa ajili ya Kristo. Ni wa kwenda chini kwa maana ya kwamba utendaji mkuu ni ule utakao juu na kuwajia wanadamu. Mungu alimchagua Ibrahimu (Mwa. 12), akawakomboa Israeli (Kutoka 14), akawaongoza kwenye Nchi ya Ahadi (Hesabu), na kuwapa maagizo kwa ajili ya kubarikiwa kwao katika nchi (Kumbukumbu la Torati). Katika Manabii, kwa upande mwingine, kuna mtazamo wa mbele katika kumtarajia Masihi, ambaye walimtazamia kwa njia ya maandalizi na unabii. Manabii walijenga juu ya msingi wa Torati ya Musa nyumba ya tumaini la Kimasihi wakiwa juu ya paa ambayo kutokea huko wangeweza kuutazamia utimilifu wa wakati ujao katika Kristo. Mashairi (Maandiko) yanaongeza mwelekeo wa tatu— mtazamo wa juu katika kuutamani ujio wa Kristo. Mengi ya yale ambayo washairi waliandika hayahusishwi moja kwa moja na ujio wa Kristo, lakini kwenye kiini cha hayo yote unaweza kuona mtazamo wa kuelekea juu, wenye kutamani kitu cha juu zaidi ambacho, kwa hakika, kilitimizwa kikamilifu katika Kristo. Wakati fulani Ayubu alimlilia mtu ambaye angeweza kuwa mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu (Ayubu 9:33); Agano Jipya linasema, “mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu” (1 Tim. 2:5). Sulemani alitamani upendo mkamilifu (Wimbo Ulio Bora); Yesu aliutoa (Yh 15:13, taz. 1 Yh 4:17-18). Kitabu cha Mithali kiliitamani hekima (rej. Mithali 8), na Kristo ndiye hekima ya Mungu (1Kor. 1:30, taz. Kol. 2:3). “Mhubiri” wa kitabu cha Mhubiri alitafuta furaha na kuridhika; Kristo alisema, “Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe” (Yh 15:11). Na hivyo ndivyo ilivyo katika “Maandiko”; kuna matamanio ya juu ya ujio wa Kristo ambayo mara nyingi hayakukusudiwa katika muktadha huo lakini yapo kila wakati na hayakutimizwa kikamilifu

91

Made with FlippingBook Digital Publishing Software