Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
katika mwingine yeyote isipokuwa katika Yule “ambaye nafsi yangu imependezwa naye.” Uenezi na Tafsiri ya Kristo Agano Jipya pia lina muundo unaofaa zaidi kwa mgawanyo wa sehemu tatu. Katika mgawanyo huo, udhihirisho wa Kristo unaonyeshwa katika Injili; Ufafanuzi juu ya Kristo katika Nyaraka; na kitabu cha Matendo kinachozingatiwa tofauti kinarekodi uenezi wa Kristo. Hii ni njia ya asili ya kugawanya Agano Jipya na imekuwa ikifanyika hivi tangu nyakati za awali katika historia ya Kanisa (ona Eusebius, Church History , III, 25). Matendo ni historia ya Kanisa la mitume na hivyo kwa kawaida iko katika fungu tofauti na Nyaraka, ambazo zilikuwa ni jumbe kwa makanisa ya kwanza (na watu binafsi). Yesu alikuwa amewekeza huduma yake ya awali kwa sehemu kubwa katika nchi yake na watu wa taifa la Israeli – Wayahudi. Alimwambia mwanamke Mkanaani, “Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli” (Mt. 15:24). Wakati Wayunani walipouliza habari za Yesu, Yesu alijibu hivi: “Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi” (Yh 12:24). Kwa hili Yesu alionyesha kwamba huduma yake kwa wakati ule ilikuwa ni kufa lakini matunda ya kifo chake yangeweza hapo baadaye kuenea kwa Wayunani. Uenezi huu wa Kristo ulipaswa kutimizwa baada ya kufufuka kwake wakati Yesu alipowaamuru wafuasi wake “enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi,” (Mt. 28:19). Maneno yake ya mwisho kabla ya kupaa yalikuwa: “…nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi” (Mdo 1:8). Kitabu cha Matendo ni rekodi ya utimilifu wa amri hii; ni simulizi ya kuenezwa kwa habari za Kristo katika ulimwengu wote. Kwanza, ujumbe wa Kristo, kulingana na amri Yake, ulienea Yerusalemu (Mdo. 2-5), kisha
92
Made with FlippingBook Digital Publishing Software