Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
katika Yudea yote (sura ya 6-7), na kisha Samaria (sura ya 8), na hatimaye katika nchi zote za ulimwengu (sura 10-28). Ingawa msukumo wa Matendo kimsingi ni wa kihistoria, Nyaraka, kinyume chake, ni za kitheolojia. Kwa hiyo, mgawanyo wa Agano Jipya katika sehemu tatu unaonyesha kwamba Kristo ambaye wakati wa maisha yake alidhihirishwa kwa Wayahudi, na ambaye katika Matendo ya Mitume habari zake zilienezwa ulimwenguni kote, ametafsiriwa au kufafanuliwa katika Nyaraka kwa ajili ya waamini.
KRISTO KAMA MSINGI: MGAWANYO WA MAANDIKO KATIKA SEHEMU NANE Msingi wa Mgawanyo katika Sehemu Nane
Wakati Agano la Kale la Kiebrania lilipotafsiriwa katika Kiyunani (linaloitwa Septuagint au LXX) huko Aleksandria, Misri (karne ya tatu, K.K. na baadaye), inaonekana kulikuwa na mpangilio mpya wa vitabu kulingana na mada zake. Vivyo hivyo, Vulgate ya Kilatini ya Jerome (karne ya nne hadi ya tano B.K) inaweka pamoja vitabu kulingana na mada zake kama Torati (Mwanzo-Kumbukumbu la Torati), Historia (Yoshua-Nehemia), Ushairi (Ayubu-Wimbo Uliobora), na Unabii (Isaya Malaki). Huu ndio mpangilio wa Agano la Kale la Kiprotestanti leo. Agano Jipya tangu nyakati za awali limeangukia katika makundi ya Injili Nne , Matendo , Nyaraka na Ufunuo , ambacho kwa kukaa kwake mwishoni, kwa namna fulani kinaunda fungu la nne, yaani, unabii wa Agano Jipya. Kwa hivyo kuanzia karne za mapema za Kanisa la Kristo hadi sasa, kwa asili Biblia nzima imeangukia katika muundo wake wa mada nane kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali inayofuata. Bila shaka, Biblia inaweza kugawanywa katika sehemu saba kwa njia mbalimbali. Jambo la maana si jinsi Biblia inavyogawanywa bali jinsi inavyohusiana. Haijalishi ni muundo gani, Kristo lazima awe mada kuu. Muundo wa sehemu nane haujaangaziwa kwa kina hapa si kwa sababu
93
Made with FlippingBook Digital Publishing Software