Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
kwa ajili ya Kristo; katika Ushairi kuna mtazamo wa kuelekea juu katika kutamani ujio wa Kristo; na katika Unabii kuna mtazamo wa kuelekea mbele katika kumtarajia Kristo. Katika Torati, Mungu anatenda juu ya watu wake ili kuweka msingi kwa ajili ya kile kinachofuata; katika Historia, taifa hilo linakuwa hai na kusonga mbele ili kuteka nchi na kuanzisha nasaba ambayo Kristo Mfalme atatokana nayo. Bila maandalizi haya kwa ajili ya Kristo, kusingekuwa na utimilifu wa matarajio na matamanio yao. Sasa muundo wa sehemu nne wa Agano Jipya unatengeneza ulinganifu wa kuvutia na mwenendo huu wenye mielekeo minne katika sehemu za Agano la Kale kama ifuatavyo: A.K Torati Historia Washairi Unabii Mwelekeo Kuelekea chini Kuelekea nje Kuelekea juu Kuelekea mbele A.J Injili Matendo Nyaraka Ufunuo Ulinganifu kati ya Torati na Injili Torati na Injili zote zina mwelekeo wa kushuka chini. Katika Torati, Mungu anashuka ili kukaa katika ulimwengu kwa namna ya mfano (mahema, Kristofania, nk.); katika Injili, Mungu anakaa ulimwenguni katika umbo la mwanadamu (Yh 1:14). Katika Torati, msingi umewekwa ili taifa la Israeli liweze kujengwa juu yake; katika Injili, Jiwe la pembeni limewekwa kwa ajili ya Kanisa kujengwa juu yake (Efe. 2:20; Mt. 16:16-18). Katika Torati kuna mhusika mkuu mmoja, Musa, ambaye anawafundisha watu haki ya Mungu; katika Injili, Kristo, Mhusika Mkuu, anafundisha wafuasi wake kuitafuta haki ya Mungu (Mt. 6:33). Ingawa Torati na Injili zote zina mwelekeo wa kushuka, na zote mbili zinaweka msingi kwa ajili ya Agano husika, na pia zote mbili zina mwalimu mkuu mmoja wa haki, bado kuna tofauti za kimsingi pia. Bila shaka kuna tofauti dhahiri iliyoelezewa hapo awali kwamba kweli ya
95
Made with FlippingBook Digital Publishing Software