Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

Agano Jipya ni kuu kuliko mafundisho ya Agano la Kale. Kisha kuna tofauti isiyopimika kati ya wahusika wakuu wa kila Agano – Kristo na Musa. Waebrania inafupisha tofauti hii kwa maneno haya: “Na Musa kweli alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama mtumishi, awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa baadaye; bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba ya Mungu…” (3:5-6). Wote wawili walikuwa waaminifu kwa nyumba ya Mungu, lakini Musa alikuwa mtumishi tu katika nyumba hiyo. Kristo alikuwa Mwana juu ya nyumba. Musa alithibitishwa kuwa mtumishi wa Mungu wakati nchi ilipofunguka na kuwameza adui zake (Hes. 16:32). Kristo aliinuliwa kama Mwana wa Mungu wakati mbingu zilipofunguka na sauti ikasema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye, msikilizeni yeye” (Mt. 17:5, taz. 3:17). Na hata Musa alikuwepo kusikiliza, na kufurahi, kwani alikuwa ameandika juu ya Kristo (Yh 5:46). Ulinganifu kati ya Historia na Matendo Historia katika Agano la Kale na Matendo ya Mitume katika Agano Jipya vina ulinganifu fulani muhimu kwa namna vinavyohusiana na Kristo. Kwanza, vyote wawili vina mwelekeo wa nje. Katika Yoshua Waisraeli wanatoka kwa ushindi juu ya ulimwengu; katika Matendo makanisa vivyo hivyo yanaitwa watu “walioupindua ulimwengu” (Mdo 17:6). Israeli ina siku zake za giza (Waamuzi), kanisa nalo pia lina matatizo yake (rej. Mdo. 5:1-; 6:1-), lakini makundi yote mawili yanaibuka washindi—Israeli kwa msaada wa manabii wao, makuhani na wafalme wenye haki (rej. Samweli Mambo ya Nyakati) na kanisa pamoja na Kristo ambaye ni Nabii wao (Mdo 3:22), Kuhani (7:55-), na Mfalme (17:7). Kadhalika, sehemu zote mbili zinaandika historia ya Agano husika, na zote zinashuhudia watu wa Mungu wakitoka nje wakiitikia mtembeo wa Mungu juu yao. Hata hivyo, katika suala hili, Matendo ya Mitume katika Agano Jipya yanapita Historia ya Agano la Kale kwa kiwango kikubwa sana. Abramu aliambiwa kwamba angekuwa taifa kubwa ambalo kupitia hilo

96

Made with FlippingBook Digital Publishing Software