Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
“jamaa zote za dunia zitabarikiwa” (Mwa. 12:3). Wajibu huu, kama njia ya baraka za Kimasihi kwa mataifa, inaonekana haukutimizwa vizuri sana na Wayahudi wa Agano la Kale. Kulikuwa na matukio kama ya kuletwa ndani kwa Ruthu au Rahabu na hata Yona aliyesitasita kutumwa nje , lakini kwa kiasi kikubwa walishindwa kuwa mfereji wa baraka kwa mataifa ya wakati ule (taz. Rum. 11:7, 15, 21). Badala ya kushirikisha baraka na ahadi za Mungu, walizihifadhi; badala ya kujenga madaraja kati yao na watu wa mataifa mengine, walijenga ukuta wa uadui, “kiambaza cha kati kilichotutenga” (Efe. 2:14). Katika Kristo na Kanisa lake, hata hivyo, ukuta huu “ulibomolewa,” na Wayahudi na Wamataifa wakawa “mtu mmoja mpya” katika Kristo (2:15). Kwa hiyo kanisa la Agano Jipya linasonga nje kuyaelekea makundi ya watu katika upana mkubwa zaidi kuliko taifa lililochaguliwa la Agano la Kale, na mwishowe litajumuisha watu kutoka katika kila taifa, kabila, lugha na jamaa. Historia ya Agano la Kale ilikuwa imetoka tu katika maana ya maandalizi kwa ajili ya Kristo; Historia ya Agano Jipya (Matendo) inaonyesha Kanisa likisonga mbele katika uenezaji wa habari za Kristo ulimwenguni. Ulinganifu kati ya Mashairi na Nyaraka Ndani ya Mashairi kadhalika ndani ya Nyaraka kuna mtazamo wa kuelekea wa juu. Washairi walitazama juu katika matamanio yao kuhusu Nabii na Mfalme ambaye angeweza kutimiza shauku za mioyo zao. Nyaraka za Agano Jipya zinamtazama Kristo, Kuhani Mkuu wa watu wa Mungu wa Agano hili, anayewapa mahitaji ya maisha yao (taz. Ebr. 4:14-16). Zaidi ya hayo, Mashairi na Nyaraka zote ni tafsiri za kweli za msingi zinazotangulia. Mashairi hayakuongeza chochote kwenye ukweli wa msingi wa matendo makuu na maneno ya Mungu yaliyoandikwa katika Torati ya Musa; badala yake, yalikuwa ni tafsiri na matumizi yake (rej. Zab. 44, 89). Kwa kielelezo, kitabu kikuu cha kishairi cha Zaburi kimegawanywa
97
Made with FlippingBook Digital Publishing Software