Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

katika sehemu tano kwa kufuata kielelezo cha mgawanyo wa Torati. Hekima ya Sulemani ni tafsiri na matumizi ya amri za Musa. Sambamba na hili, Nyaraka ni ufafanuzi wa maneno na matendo makuu ya Kristo yaliyoandikwa katika Injili. Kweli ya Mitume wote inajengwa juu ya mafundisho ya Kristo. Mafundisho yao yamejengwa juu ya matendo na maneno ya Kristo. Ni kweli kwamba Mashairi kadhalika Nyaraka zinaeleza wazi kile ambacho Musa na Kristo walimaanisha, lakini si mitume wa Agano Jipya wala manabii wa Agano la Kale wanaoeleza yale ambayo watangulizi wao hawakuwa wametabiri mahali fulani. Mashairi na Nyaraka pia zinaweka matumaini yake juu: Mashairi yakitazama juu kwa shauku ya kumwona Yeye ambaye bado hajaja, na katika Nyaraka watu wa Mungu wanamtazama Yeye ambaye ametoka tu kuondoka na sasa anaishi juu kabisa ili kuwaombea (Ebr. 7:25). Ulinganifu kati ya Manabii na Ufunuo Manabii wa Agano la Kale na kitabu cha Ufunuo katika Agano Jipya vina uhusiano ulio dhahiri: Vyote ni unabii wa Kristo. Vyote vinatazamia ujio wa Kristo: Agano la Kale linatazamia ujio wake wa kwanza na wa pili, na Agano Jipya likitazamia ujio wa pili wa Kristo (Ufu. 1:7; 22:12). Ni sahihi kabisa kwamba maagano yote mawili yanamalizika kwa matarajio yanayofanana, lakini pia kuna tofauti muhimu. Jambo moja ni kwamba, nabii Danieli wa Agano la Kale aliambiwa, “Enenda zako, Danielii; maana maneno haya yamefungwa, na kutiwa muhuri, hata wakati wa mwisho” (Dan. 12:9). Yohana, kwa upande mwingine, aliambiwa, “Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia” (Ufu. 22:10). Manabii wa Agano la Kale walitazamia kwa hamu siku ambayo Kristo angefungua gombo la unabii. Ufunuo katika Agano Jipya unatazamia utimilifu wa mambo yote katika Kristo, ambaye yuko karibu kuzifungua mihuri za unabii. Jambo kubwa zaidi ni kwamba manabii wa

98

Made with FlippingBook Digital Publishing Software