Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
Agano la Kale walipata hapa na pale mafunuo juu ya Kristo ajaye; Yohana alipokea “Ufunuo wa Yesu Kristo” (Ufu. 1:1). Katika fumbo linalohusiana na ufasiri wa kitabu cha Ufunuo, labda kuna kosa moja tu hatari sana—kutoweza kuona kwamba kitabu hicho si fumbo la kiunabii linalohitaji kuunganishwa na mkalimani mwerevu; ni ufunuo wa Yesu Kristo. Ufunuo huu unatuambia kwamba Yeye ambaye Musa aliweka msingi kwa ajili yake, ambaye historia ya Israeli ilimwekea matayarisho, ambaye washairi na manabii walimtazamia kwa shauku na matarajio makubwa, na ambaye udhihirisho wake umo katika Injili, uenezaji wa habari zake katika Matendo na tafsiri yake katika Nyaraka, atakuwa lengo la mwisho na utimilifu wa mambo yote pia.
99
Made with FlippingBook Digital Publishing Software