Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
/ 2 4 9
K U T A F S I R I B I B L I A
K I A M B A T I S H O C H A 1 7 Nadharia za Uvuvio Mch. Terry G. Cornett
Nadharia za Uvuvio
Maelezo
Pingamizi zinazowezekana kuwepo
Mwandishi wa kibinadamu ni kifaa mikononi mwa Mungu kisichokuwa na athari. Mwandishi anaandika tu kila Neno kama Mungu anavyoliongea. Uandishi huu wa moja kwa moja ndio unaozuia andiko kuwa na makosa ya kibinadamu.
Vitabu vya Biblia vinaonyesha utofauti katika aina za uandishi, msamiati, na namna za kujieleza ambazo zinatofautiana kutoka kwa mwandishi mmoja na mwingine. Nadharia hii haionyeshi kuelezea kwanini Mungu alitumia waandishi wa kibinadamu badala ya kutupa Neno lililoandikwa moja kwa moja kutoka kwake mwenyewe. Biblia inaonyesha kwamba Maandiko yalitoka kwa Mungu, kupitia waandishi wa kibinadamu (2 Pet. 1.20-21). Maandiko yanaonyesha kwamba waandishi wa kibinadamu waliwasilisha Neno halisi la Mungu (hasa maandiko yanayoonyesha maneno “asema Bwana”; Rum. 3.2.) Waandishi wa Biblia kamwe hawajawahi kuonyesha kwamba Maandiko fulani yamevuviwa zaidi au kushughulika na aina moja tu ya Maandiko kama ndio iliyovuviwa katika matumizi yao. Yesu anaongea kuhusu ufunuo wote wa Maandiko hadi kufikia nyakati zake kwamba ni Neno toka kwa Mungu lisilobadilika (Mt. 5.17-18; Yohana 3.34-35). Inaonekana kama vile haiwezekani kwamba vipengele vya kibinadamu ambavyo vina mwisho wa matumizi yake na vyenye mafungamano na utamaduni fulani tu vingeweza kuelezewa kama Neno la Mungu lisilobadilika.
Nadharia ya Uvuvio wa Kiimla
Nadharia ya Uvuvio wa Kihisia au Wa Asili
Watu wenye karama na maono ya kipekee ya kiroho walichaguliwa na Mungu kuandika Biblia.
Roho Mtakatifu aliongeza kimo cha uwezo wa kawaida wa uelewa wa waandishi wa kibinadamu ili kwamba wawe na maarifa ya kipekee kuhusu kweli za kiroho.
Nadharia ya Kuangaziwa
kwa maandiko (Illumination)
Sehemu fulani za Biblia zimevuviwa zaidi kuliko nyingine. Wakati fulani sehemu hii huwa inatumika kujadili kwamba sehemu za Biblia zinazohusika na mafundisho ya msingi na kweli za kimaadili zimevuviwa zaidi, wakati sehemu za Biblia zinazohusika na historia, uchumi, utamaduni n.k zimevuviwa kidogo au hazijavuviwa kabisa. Viashiria vyote vya kimungu na kibinadamu vipo katika uzalishaji wa Maandiko. Maandiko yote ya Biblia, pamoja na maneno yote, ni zao la ufahamu wa Mungu ulioelezewa kwa namna na hali ya kibinadamu, kupitia waandishi wa kibinadamu ambao aliwafahamu tangu Mwanzo (Yer. 1.5) na kuwachagua kwa ajili ya kazi yake.
Nadharia ya Viwango vya
uvuvio (au Uvuvio wa sehemu)
Nadharia ya Uvuvio wa
neno kwa neno – Uvuvio Kamili
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker