Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
/ 3 2 7
K U T A F S I R I B I B L I A
Masomo ya Biblia Kutumia Zana za Kujifunzia Katika Kujifunza Biblia
MAELEZO YA MKUFUNZI 4
Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi kwa ajili ya Somo la 4, Masomo ya Biblia: Kutumia Zana za Kujifunzia Katika Kujifunza Biblia . Shabaha kuu katika somo hili ni manufaa ya zana ambazo uhakiki wa Biblia wa sasa umetoa kwa mwanafunzi mwenye bidii na njaa ya kujifunza Biblia. Wakati uhakiki wa Biblia mara nyingi umekuwa ukija na hitimisho ambalo labda linapingana moja kwa moja au kuona kama tafsiri ya moja kwa moja ya Biblia kama iliyotiwa chumvi na isiyoweza kujitetea, nyenzo nyingi zinazotengenezwa na wanazuoni zina manufaa sana kwa kujifunza Biblia. Leo hii, kazi nyingi za namna hii, zikiwa ni mazao ya miaka mingi ya utafiti katika lugha, historia, na utamaduni wa ulimwengu wa Biblia, zinapatikana kwa gharama ndogo sana. Kwakweli ni kipindi adimu sana hasa kwa mwanafunzi ambaye anataka kuzipata kazi bora kwa kila awamu ya kujifunza Biblia na theolojia pia. Uhakiki wa Biblia ni nini hasa kwa ufupi, ni nidhamu gani zinahusika, na ni nini malengo yake kuhusiana na kujifunza Biblia yenyewe? Mwandishi, G. J. Wenham anatoa jibu kwa ufupi: Uhakiki wa Biblia leo, unahusisha taaluma mbalimbali ambazo lengo lake ni kutafsiri Biblia kwa ufasaha unaohitajika. Aina nyingi za uhakiki zinalenga kueleza zaidi maana ya andiko: Na hauko katika namna ya kukosoa andiko au maana yake. Kwa asili uhakiki wa Biblia umekuwa ukihusika sana na masuala ya kihistoria: Nani aliandika andiko? Liliandikwa lini? Ni makosa gani yanaweza kuwa yaliingia kupitia kunakili? Vyanzo gani vilitumika? n.k. mambo haya bado ni masuala ambayo wanazuoni wengi bado wanayashughulikia, lakini kwa kuongezeka sana mifumo mingine ya uhakiki inatokea. Uhakiki huu wa kisasa unalenga zaidi kwenye andiko lenyewe au kwa msomaji. Uhakiki unaohusiana na andiko ni pamoja na balagha, kanuni, na uhakiki mpya, wakati uhakiki unaohusiana na msomaji unahusisha hadhira, mbinu za mitazamo ya kiukombozi na ufeministi. ~ G. J. Wenham. “Biblica Criticism” The New Bible Dictionary . D. R. W. Wood, ed. 3rd ed. (Electronic Ed.). Downers Grove, IL: Intervarsity Press, 1996, uk. 138. Ufafanuzi huu unatoa ufafanuzi unaeleweka wa taaluma ambazo zimezalisha safu kubwa ya zana za kuaminika kwa ajili ya kujifunza Biblia. Pia, wakati zana za maungamo na theolojia za uhakiki huria zinajaribu kukataa ukweli wa kihistoria wa madai ya Biblia, nyenzo nyingi zaidi za kihistoria, kijamii na kitamaduni zinatoa ufahamu wa kuvutia na wenye msaada mkubwa katika ulimwengu wa Biblia.
1 Page 169 Utangulizi wa Somo
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker